Latest News


More

HEKIMA ITUONGOZAYO KATIKA UFALME WA MUNGU

Posted by : Unknown on : Monday, July 29, 2013 0 comments
Unknown
 Askofu Makala akihubiri kwenye ibada ya jumapili katika Usharika wa Ebenezer kanisa kuu la K.K.K.T alisema  hekima ituongozayo wakristo inatakiwa itoke katika ufalme wa Mungu na wala si hekima ya kutegemea akili zetu wenyewe
Na hekima ni Kristo mwenyewe.Askofu Makala alisema hata wana wa Israelk walipungukiwa na hekima ya Mungu ndio maana waliadhibiwa mara kwa mara

Katika bada hiyo iliyokuwa pia na huduma ya chakula cha bwana ilihudumiwa pia na mchungaji kiongozi wa Usharika wa kanisa kuu, shemasi pamoja na mchungaji mwanafunzi Ordolus Gyunda
Askofu Makala akihubirti kwenye ibada hiyo mjini Shinyanga

 
Askofu Makala alisema kuna hatua mbalimbali zinazofanya wakristo haswa wanandoa kukosa hekima na upendo wa kimungu na kuanza kuwa na kiburi.Alizitaja hatua hizo za kuwa na kiburi kuwa ni kama;

1.Hatua ya kwanza ni ubinafsi katika familia kati ya mme na mke.Mume anasema hiki changu na mke naye anasema hiki changu.Hakuna ushirika wa mali au vitu wanavyovimiliki pamoja

2.Hatua ya pili ni hali ya kutotambua kosa na kuwa tayari kutubu

3.Hatua ya tatu ni hali ya kukosa mawasiliano kati ya mke na mume au mume na mke

4.Hatua ya nne ni kutokuaminiana kati ya mke na mume.Unajiamini wewe mwenyewe

Mwisho wa hayo yote ni utengano – Isolation

Lakini hekima ya Kimungu ikiwepo hayo yote hayawezi kuwepo alihitimisha Askofu Makala




Mchungaji kiongozi wa Usharika wa kanisa kuu

 Wanakwaya wa kwaya ya Vijana wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu wao Askofu Makala mara baada ya ibada hiyo

No comments:

Leave a Reply