Wataalamu wa macho kutoka nchini Marekani wako mjini
Shinyanga wakitoa ushauri wa kitaalamu wa macho na pia miwani kwa wale wanaoonekana kuwa wanahitaji miwani
Wataalam hao ambao wamekuja nchini kwa mwaliko wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini y a Ziwa Victoria Usharika wa
Ebeneza lililoko Shinyanga Mjini
Matibabu hayo ambayo yanatolewa kwenye zahanati ya Usharika huo iliyoko katika eneo la Usharika wa Ebeneza yanatolewa kwa gharama kidogo tu ya shilingi
2500 kama ada ya kujiandikisha na kisha miwani inatolewa bure kwa wale wanaoonekana wanahitaji kupewa miwani
Wataalamu hao watakuwa mjini hapo kwa muda wa siku tano kuanzia jumatatu ya wiki hii.
Pichani wataalamu wakiwapima macho watu waliofika kituoni hapo
Mtaalamu wa macho akimwelekeza mgonjwa kusoma alama zilizoko kwenye ubao mbele
No comments: