MAWAZIRI, wabunge, maaskofu, mapadri, wachungaji wanaohusika
uagizaji na uuzaji dawa za kulevya wametakiwa kutubu, kujisalimisha kwa Rais
Jakaya Kikwete, ndani ya wiki hii vinginevyo majina yao kusambazwa katika
balozi zote duniani.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga, kutokana
na wanafunzi wawili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na St.Gasper cha
Morogoro kusalimisha kilo tano za heroine katika kongamano la kidini
lililofanyika TAG Mbeya.
Mbali na kujisalimisha vijana hao
walitaja mawaziri wawili, Naibu waziri mmoja, wachungaji, baadhi ya wabunge
watatu wa viti maalum na wabunge wastaafu wanaomiliki biashara kubwa ndani na
nje ya nchi.
Mchungaji Mwamalanga alisema
wamesikitishwa na viongozi hao wakuu wa nchi ambao ndio wanatakiwa kuonesha
mfano kwa Watanzania kupiga vita dawa za kulevya, lakini wao ndio vinara wakuu
wa kuwatumia vijana hao kununua na kuyauza kinachoshangaza zaidi ni watumishi
wa dini, maaskofu, wachungaji nao kuhusika na biashara hii kwa kutumia jina la
Mungu kwa namna tofauti na sote tunaonekana tunafanya hivyo,"alisema.
Mchungaji Mwamalanga alisema wiki hii ni ya viongozi hao wa dini
na serikali kutubu kwa ukamilifu mbele za Mungu na ikiwezekana waache kazi
hizo, kwani hawaitakii mema nchi na Taifa lote kwa ujumla."Hii wiki ya
kutubu kwa mawaziri na wabunge waliotajwa pamoja na kutubu wajisalimishe
wenyewe kwa Rais Jakaya Kikwete wamweleze kwamba wao ni mabingwa wa kuuza dawa
za kulevya.
"Kama hawatafanya hivyo wiki ijayo tutaanika majina yao yote
katika balozi mbalimbali duniani kwamba hawa ndio vinara wa dawa za kulevya
Tanzania, hivyo wakifika katika nchi hizo wasiruhusiwe kufanya chochote
wakamatwe," alisema.
Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa kusudi la kuanika majina yao ni
ili dunia iwatambue na kusisitiza kwamba wasipofanya hivyo wiki ijayo
watasambaza majina yao duniani kote.
Alisema kuwa viongozi hao wa dini wanatakiwa kujitambua na ndipo
waweze kutubu ili waweze kupokea nguvu ya Mungu kwa kutubu mbele zake.
Mc h u n g a j i Mwama l a n g a a m e w a o m b a m a a s k o f u
, wachungaji, mapadri, mashekhe kuungana pamoja kuwafichua wenzao wanaohusishwa
na tuhuma hizo kwa kuwa wanajulikana.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Moroviani Iringa Abeid Mbisa alisema
aliwashutumu viongozi hao wa dini kwa kutumia jina la Yesu vibaya na kwamba
watumishi wote wa dini wanahusishwa na kashfa hiyo wakati hawahusiki.
"Wanatumia jina la Yesu vibaya ninawashauri wapumzike kufanya
kazi ya Mungu na badala yake wafanye kazi nyingine na ikiwezekana watubu na
kumtumikia inavyopaswa,"alisema.
Alisema vijana wamekuwa wakiharibiwa na watu ambao hawakuwategemea
na badala yake wanapaka matope makanisa na Taifa zima kwa ujumla.
Naye Mchungaji wa Kanisa la TAG, Calvary Tempo, Daud Mwalonde
alisema kitendo cha viongozi hao wa dini, pamoja na viongozi wa serikali
kuhusishwa katika sakata hilo la dawa za kulevya kunadhoofisha nguvu ya Taifa.
Alisema vijana wanalala barabarani,
wanakuwa na sauti ambazo sio zao na nguvu ya Taifa imekwisha
kutokana na wengi kupoteza nguvu ya kufanya kazi kutokana na kutumiwa vibaya.
"Ombi langu kama mtu ameamua kuwa mtumishi afanye kazi ya Mungu asifanye
Taifa kuelekea pasipotakiwa na kama mtu ni mchungaji na kisha anashiriki kazi
hizi aachane na huduma hiyo kwa sababu haitakii mema Tanzania," alisema.
Wakati huo huo, Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,
imesema ina majina ya vigogo ambao wanahusika na uuzaji na usambazaji wa dawa
hizo ambapo wanachunguza kwa kina na pindi upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa
kukabidhi msaada wa fedha wa kiasi cha sh.milioni 2.5 kwa taasisi zisizo za
kiserikali za Tandika Youth Handcraft Group (TAYOHAG) Kwaya ya Nazareti,
Kamishna wa tume hiyo, Christopher Shekiondo, alisema kazi ya kupambana na dawa
za kulevya inafanyika vizuri na kwamba hadi sasa wana majina ya vigogo
wanaojihusisha na dawa hizo, lakini wanaendelea na upelelezi.
Alisema
baadhi ya vigogo hao wengine watafikishwa mahakamani wengine wamekimbia nchi na
wengine bado hawajakamatwa na wanaendelea kuw atu miavijana kufuata dawa
hizonjeya nc hi.
“Tuna
majina ya vigogo ambao wanajihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, lakini
hatuwezi kuwataja kwa majina kwa sababu lazima kwanza tufanye upelelezi wetu wa
kina ili tuwakamate na kama wamefikishwa mahakamani hatuwezi kuwataja hadi kesi
iishe na wananchi wengi wanataka kujua majina hayo ya vigogo,” alisema.
Alisema
watu wanaokamatwa na dawa hizo ni wale wanaotumwa na vigogo hao na ndiyo
wanaokumbana na mkono wa sheria kwani wabebaji wote ndio wanaokamatwa mara
nyingi.Hata hivyo imekuwa vigumu kunasa wahusika wakuu ambao ndio wanaowatuma
wasafirishaji hao. Alisema si kila Mtanzania anayekamatwa nje ya nchi akiwa na
dawa za kulevya hutokea Tanzania, bali kutokana na wahusika kuwa na mtandao
mkubwa ndani na nje ya nchi, wanachokifanya hutuma pesa ambapo mtu anaweza
kutokea nchi nyingine akaenda Brazil na kisha kuchukua dawa hizo na kuziingiza
nchini China.
Alisema
hata hao wanaoingiza dawa hizo nchini wanapita viwanja mbalimbali vya ndege vya
kimataifa hadi kufikia hatua ya kukamatwa. Alisema mwaka 2010 kumekuwepo na
ongezeko kubwa la ukamataji wa dawa hizo za kulevya nchini wakiwemo vigogo
kutoka nje ya nchi. “Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2012 kumekuwa na ongezeko
kubwa la ukamataji wa dawa hizo ambapo kiasi cha dawa hizo aina ya heroin
kilikamatwa kilo zaidi ya 760 huku cocaine zilizokamatwa zikiwa zaidi ya kilo
340 huku takwimu zikonesha kuwa mwaka huu kila wiki dawa hizo hukamatwa,”
alisema Shekiondo.
Pamoja
na juhudi hizo lakini kuna vyombo vingi vinavyohusika na udhibiti wa dawa hizo
hivyo lazima kila sehemu inayohusika na kazi hiyo iangaliwe ili kudhibiti
zaidi.Alisema Watanzania 110 wamekamatwa nchini Brazil ambapo walikwenda
kuchukua dawa hizo na wengine 35 wamekamatwa nchini China.
Naye
Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, ameitaka
Serikali kuwakamata vigogo wote waliotajwa katika kashfa hiyo.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Mrema alisema Tanzania inaiga sera za watu wa Marekani, h
i v y o i k umb u kwe k uwa Marekani ilimkamata Jenerali Manuel Noriega
aliyekuwa Rais wa Panama kwa kuunga mkono matumizi ya dawa za kulevya nchini
mwake."Hivyo ni jukumu la Serikali, kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja
na kuruhusu sheria kuchukuwa mkondo wake kwa wahusika wote kwani ni aibu kwa
Taifa,"alisema Mrema.
Akifafanua
zaidi alisema kama Serikali haijachukua hatua za haraka ikumbuke kuwa kashfa
hiyo ndio iliyosababisha kupinduliwa kwa Serikali ya nchi ya Panama na kuongeza
hata mataifa mengine yatatuchukia kwa kuendelea kukaa kimya.Alisema hata kama
taarifa hizo hazina ukweli wa asilimia 100, lakini zina ukweli wa asilimia 80
na kuongeza kuwa kama wanataka ushahidi wa asilimia 100 basi wasubiri mpaka
atakaporudi Yesu au Mtume Muhammad ili awathibitishie.
Alisema
hali imekuwa mbaya sana katika nchi yetu, watu walionekana wakisafirisha Twiga
kupitia uwanja wetu wa ndege na sasa wameamua kusafirisha dawa za kulevya,
kupitia nchini.Mrema amevitaka vyombo vya habari kutaja hadharani majina ya
watu wote wanaojihusisha na mtandao huo ili kutoa fundisho kwa wahusika
wengine.
"Imefika
wakati lazima tuwe majasiri kwa kuwataja majina hadharani, potelea mbali
tutawaomba samahani baadae maana sasa hali inatisha,"alisema Mrema.Alisema
ikiwa mawaziri na wabunge wanatajwa kuhusika na dawa za kulevya, halafu wenyewe
wanakataa wakidai wanasingiziwa ni lini watakubali ukweli kila siku
wanasingiziwa wao tu.
No comments: