WATOTO WA SHULE YA JUMAPILI WAZAWADIWA KWA KUFAULU MITIHANI YAO
Watoto wa shule ya jumapili katika Usharika wa K.K.K.T Usharika wa Mwenge walizawadiwa zawadi mbalimbali kwa kufaulu mitihani yao ambayo waliifanya kwa ngazi ya Usharika na baadaye Kufanya mitihani ya ngazi ya jimboPamoja na hao waliofaulu mitihani kuzawadiwa pia kuna waliozawadiwa kwa kuwa na nidhamu wawapo darasani.Pichani juu ni mtoto mwenye nidhamu kuliko wengine akipewa zawadi yao na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge.Kushoto kwake ni katibu wa baraza la wazee mzee Kombe na pembeni yake mwenye tai nyekundu ni mzee Uronu
Mama Vanesa Ndosi akimpokelea zawadi mtoto wake aliyefaulu vizuri.Mwanae alikua wa pili kwa kundi la watoto wa miaka 1 - 2 kwa kupata alama 70
Katika zawadi hizo kulikua na Makundi yafuatayo;
KUNDI LA KWANZA - MIAKA 1 - 2
Mshindi wa kwanza Agnes Chavala alama 80
Mshindi wa pili Vanesa Ndosi alama 70
Mshindi wa tatu Tety Moses alama 60
KUNDI LA PILI – MIAKA 3 – 4
Mshindi wa kwanza Maria Peter alama 85
Mshindi wa pili Simbele Sukuru alama 84
Mshindi wa tatu Ema Godson alama 78
KUNDI LA TATU MIAKA 5 – 7
Mshindi wa kwanza Eva Raymond alama 80
Mshindi wa pili Lisa Mwuta alama 74
Mshindi wa tatu Ivin Somi alama 72
No comments: