Latest News


More

KWAYA UINJILISTI KIJITONYAMA YAZINDUA ALBUM YA "NAMTANGAZA KRISTO" LEO

Posted by : Unknown on : Sunday, October 13, 2013 0 comments
Unknown


Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama maarufu kama "KIJITO" leo imefanya tamasha kubwa la uimbaji katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharikani kwao Kijitonyama
Pichani  juu ni mwenyekiti wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama akiwa na mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchubgaji Kadiva
Tamasha hilo ambalo limefanyika sambamba na uwekaji wakfu wa album yao mpya yenye jina "NAMTANGAZA KRISTO' tendo ambalo limefanyika katika ibada zote tatu Usharikani kwao
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikua askofu msaidizi wa DMP mchungaji Fupe

 Modest Morgan muimbaji kiongozi wa kwaya ya Uinjilisti akiimba kwenye uzinduzi huo
 


 

Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama mchungaji Ernest Kadiva akizungumza wakati wa tamasha la uzinduzi wa DVD na CD ya kwaya ya Kijitonyama leo mchana 

Baada ya ibada kwaya yaUinjilisti Kijitonyama imefanya tamash kubwa la nyimbo za injili ambalo limeshirikisha kwaya na waimbaji mbalimbali kama vile;
1.Upendo Nkone
2.Mariam Lukindo
3.Kwaya ya AICT Chang'ombe na
4.Kwaya ya Uinjilisti Kigogo
Kwaya zote zilizoalikwa pamoja na waimbaji waliimba nyimbo mbili kila moja live
SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU!!

Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa Blog

No comments:

Leave a Reply