Latest News


More

MCHUNGAJI LAWRENCE KYAKA WA K.K.K.T AZIKWA LEO HUKO MKUZA

Posted by : Unknown on : Wednesday, October 16, 2013 1 comments
Unknown




MCHUNGAJI LAWRENCE KYAKA WA K.K.K.T AZIKWA LEO HUKO MKUZA

Mchungaji  Lawrence Kyaka aliyefariki siku ya jumamosi  tarehe 12/10/2013  amezikwa leo  huko Mkuza kwenye samba lake 

Ibada ya kumwaga imeanza katika Usharika wa Msewe ambao ndio aliotumika mpaka mauti ilipomfika na baadaye tena ibada ikaendelea kwenye Uharika wa Mkuza  ambapo pia aliagwa na kisha kwenda kupumzishwa kwenye shamba lake lililopo maeneo ya Mkuza

Mchungaji Kyaka ambaye alikua akihudumu katika Usharika wa  Msewe mpaka umauti ulivyomfika alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa Kansa kwa muda mrefu na kutibiwa katika hospitali mbalimbali kama vile Muhimbili na India 

Ibada ya mazishi imeongozwa na  Askofu na mkuu wa kanisa la DMP na mkuu wa kanisa la K.K.K.T Dr Alex Malasusa , askofu mstaafu  wa DMP Mzee Sendoro , maaskofu mbalimbali  na kuhudhuriwa na maelfu ya waumini na viongozi mbalimbali wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na kanisa la K.K.K.T na makanisa mbalimbali
Marehemu ameacha  mjane na watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike
MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI…AMEN

1 comments: for MCHUNGAJI LAWRENCE KYAKA WA K.K.K.T AZIKWA LEO HUKO MKUZA