Malasusa:Ni vema zikajengwa nyumba za ibada nyingi kuliko magereza
Ikiwa ni mfululizo wa matukio ya kuchomwa moto makanisa na matukio mengine yanayopelekea uvunjifu wa amani mkuu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania Dk Alex Malasusa ameongoza ibada maalum ya ufunguzi wa nyumba ya ibada ya usharika wa Mabibo Exteral jijini Dar es salaam huku askari wenye silaha za moto wakiwa nje ya jengo hilo.
Katika ibada hiyo kulikua na askari wenye silaha za moto wakizunguka huku na huko katika jengo hilo na gari mbili za polisi zikiwa zimeegesha pembeni mwa kanisa hilo ikiwemo landrover ya OCD Kimara huku ibada ikiendelea ndani
Akizungumza katika ibada hiyo Dk Malasusa amesema ni vyema kama zingekuwa zinajengwa nyumba za ibada zaidi badala ya sasa yanavyojengwa magereza vile magereza hayatoshi kumbadilisha mtu bali mtu ajengwe kwa imani ajifunza kuyataunza mazingira yanayomzunguka .
Naye mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa usharika huo Bw Ayo Urassa amesema ujenzi wa kanisa hilo ulianza mwaka 1991 na hadi unakamilika umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: