Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T ) - Usharika wa Mwenge unaandaa kufunga ndoa za pamoja mwishoni mwa mwezi November mwaka huu
Akizungumza kwenye ibada ya jumapili mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi alisema mpaka sasa hivi tayari washarika 7 wamekwishajiandikisha kufunga ndoa hizo za pamoja
Ndoa hizo zitafungwa katika Usharika huo siku ya jumapili na baada ya ibada kutakua na tafrija ya pamoja ya ndugu, jamaa na marafiki wa maharusi hao pamoja na washarika wote wa Usharika wa Mwenge, na inatarajiwa itahudhuriwa na watu wasiopungua 1000
Tayari kamati ya maandalizi ya ndoa hizo imekwisha undwa ambayo itakua na wajumbe takribani 21 na itaongozwa na wazee wa kanisa wawili ambao ni Dr Lilian Kitunga na Tumaini Kichila.
Mchungaji Kaanasia aliwaambia washarika nafasi bado ipo kwa wote ambao hawajatengeneza maisha yao na Mungu na wawe huru kufika ofisini kufunga ndoa.
Washarika naomba tuiombee sana tendo hili kubwa ambalo ni la kimungu alisisitiza mchungaji Kaanasia Msangi
No comments: