Akihubiri katika ibada ya jumapili ya leo katika Usharika wa Mwengemchungaji Ernest Kadiva wa kanisa la K.K.K.T amesema kuna changamoto nyingi zinazikabili familia zikiwepo;
1.Upendo kupoa pale ambapo na kipato kinapopungua
2.Teknolojia inachangia watoto kuharibika au kutotii mafundisho toka kwa wazazi na kanisa kwa ujumla
3.Familia kukosa nafasi ya kukaa pamoja (baba, mama na watoto) kutokana na mihangaiko ya kutafuta kipato hivyo kuchangia maadili ya watoto kuzidi kumomonyoka
Katika ibada hiyo kulikua na matendo mbalimbali yaliyofanyika kama vile kurudi kundini, ubatizo wa watoto wadodo, kipaimara kwa mkristo mmoja, shukrani za pekee, na ndoa mbili ambazo zimefungwa hivi leo Usharikani hapo na kisha kujumuika kwa chakula cha pamoja kwa washarika wote
Kwaya na vikundi mbalimbali vilijumuika kuimba ikiwepo kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge , kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza na mwimbaji binafsi mmoja
Kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza ikihudumu kwenye ibada hiyo jumapili ya leo
Waumini wakifuatilia ibada ya leo jumapili katika Usharika wa Mwenge
Katibu wa baraza la wazee wa Usharika wa Mwenge akifuatilia ibada hiyo.Pembeni ni mzee wa kanisa mama Seka Urio
No comments: