MHESHIMU BWANA KWA MALI YAKO
Mchungaji mama Mjema (pichani juu) akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Mwenge amesemaMungu anapenda aheshimiwe kwa kila kitu ambacho anatupatia
Katika ibada hii ambayo ilikua ni maalumu ya kumtolea Mungu mavuno iliyoongozwa na neon la Mungu toka Mithali 3:9, alisema unapoingia kwenye mavuno ni heshima kumtolea Mungu kile kitu chathamani kubwa ambacho Mungu amekujalia kuwa nacho
Mungu ndiye muumbaji wa yote tuliyo nayo lakini anataka umheshimu kwa mali alizokupa.
Malia unayotoa leo, ebu jiulize inampa Mungu utukufu (heshima)?
Heshima ya mali aliyokupa Mungu anataka mimi na wewe umrudishie kama heshima ya kutambua kwamba yeye ndiye muumbaji wa vyote na ndiye aliyetupa
Kumrudishia Mungu heshima kwa kumpa mali kama mavuno ni kutambua ukuu wake kwa jinsi alivyokusitiri, alivyokuvusha kwenye magumu mbalimbali aliyo, alisisitiza mchungaji mama Mjmea
Mchungaji mama Mjema ni mke wa Askofu wa Dayosisi ya Pare Askofu Mjema
Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Kaanasia Msangi
Waumini mbalimbali (pichani juu na chini) wakiwa kwenye ibada ya alfajiri (inayoanza saa 12.00 mpaka saa 1.30 asubuhi)
Katika Ibada hiyo washarika wa Mwenge walimtolea Mungu vitu mbalimbali kama vile mifugo , mazao ya shambani pamoja na fedha taslimu kama mavuno yao kwa bwana kwa mwaka huu 2013
No comments: