Ni tatizo linalotokana na kuwepo kuumizwa kwa ini kwa muda
mrefu, kutokana na visababishi mbalimblai, Ini hilo lililoumizwa kwa
muda mrefu huwa na makovu yaliyotapakaa karibu ini zima na kulifanya
lisinyae na mwisho kushindwa kufanya kazi.
Mgonjwa
huweza kukaa na tatizo hili kwa muda mrefu bila kutokuwa na dalili na
inaweza kufahamika pale anapofanyiwa vipimo hospitali hasa ultrasound
kuangalia ugonjwa mwingine (incidental findings), takriban asilimia 40
ya wagonjwa huwa hawana dalili. Dalili hizo za kusinyaa kwa ini ni
pamoja na mwili kukosa nguvu, kukonda, kutapika damu, kujaa maji
tumboni, kuvimba miguu, kuchanganyikiwa, kwa wanaopata dalili kama
kujaa maji tumboni, kutapika damu au kupata choo chenye damu, cheusi au
kuchanganyikiwa nafasi ya kuweza kuishi zaidi ya miaka mitano ni
asilimia 50, hii ina maana wengi hufariki chini ya miaka hiyo.
Mambo
ambayo husababisha Ini kuumia kwa muda mrefu na hivyo kusinyaa na
kushindwa kufanya kazi ni pamoja na kunywa pombe kali au kupitiliza,
virusi vinavyoshambulia Ini, kichocho, dawa, kemikali zenye sumu,
magonjwa ya kurithi yanayoshambulia Ini, kinga za mwili kupoteza
mwelekeo na kuanza kushambulia Ini.
Vipimo
kadhaa huweza kubaini ukubwa wa tatizo hili, kama vile ultrasound,
vimeng’enyo vya ini kupitia kupima damu, kupima uwepo wa virusi ini, CT
scan na hata MRI ingawa vipimo hivi ni gharama kubwa sana na
havipatikani kirahisi.
Matibabu
ya ugonjwa huu ni upasuaji wa kubadilisha ini na kuwekewa ini la mtu
mwingine ( Liver Transplant ) ni wazi upasuaji huu haufanyiki hapa
nchini, hufanyika katika hospitali zenye uwezo mkubwa nje ya nchi. Pia
upatikanaji wa ini la mtu mwingine ni kazi sana, kwani huhitaji mtu
huyo awe amepoteza maisha (mfano labda amepata ajali na kufariki hivyo
ini lake kutolewa haraka kuhifadhiwa na kuwekewa yule ambaye ini lake
limesinyaa na halifanyi kazi). Aidha wanasayansi wanahangaika kutafuta
dawa ya kuzuia makovu hayo kutokea kwenye ini na hivyo kufanya lisinyae.
Damu
zote anazoongezewa mgonjwa hutoka katika maabara za Serikali
zijulikanazo kama ‘damu salama’, damu hizi huwa zimefanyiwa uchunguzi
wa kina kukwepa kumdhuru mgonjwa)
No comments: