Kichinjio cha kwanza cha Punda nchini Kenya kinatarajiwa kuanza kutumika mwezi Machi wakati kitakapokamilika.
Wakaazi wa mji wa Naivasha nje kidogo ya mji
mkuu Nairobi watakuwa wa kwanza barani Afrika kuwa na kinjichio cha
punda ambao wamekuwa wakiwatumia kwa kukeba maji.Kwa muda mrefu mizoga ya wanyama hao imekuwa ikipatikana kando ya barabara au msituni ambako wezi huificha baada ya kuwachinja Punda hao.
Lakini sasa haya yote yatakuja kuisha baada ya mradi wa ujenzi wa kichinjio cha Punda kuanza mjini humo.
Kichinjio hicho kitakuwa cha kwanza na cha kipekee Kenya na Afrika Nzima cha nyama ya Punda.
Taarifa zinasema kuwa nyama hiyo tayari ina hitaji kubwa nchini China.
No comments: