Latest News


More

MARUFUKU KUVAA MINI SKIRT NCHINI UGANDA

Posted by : Unknown on : Wednesday, February 19, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .




Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.

Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.

Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.

No comments:

Leave a Reply