Latest News


More

ASKOFU WA ANGLIKANA DODOMA GODFREY MDIMI MHOGOLO AFARIKI DUNIA

Posted by : Unknown on : Friday, March 28, 2014 2 comments
Unknown

 


Dodoma. Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo amefariki dunia akiwa kwenye matibabu huko nchini Afrika Kusini Katibu wa Dayosisi ya Dodoma Luteni Mstaafy Daudi Kandila alithibitisha jana kutokea kwa kifo hicho na kusema kimeacha pengo kubwa katika Dayosisi na Kanisa Anglikana kwa ujumla
Askofu Mhogolo atakumbukwa  kwa umahiri wake wa kusimamia hoja zake kwenye vikao na kuwa askofu wa Dayosisi hii kwa miaka mingi.
Mhogolo amekuwa Askofu wa Dayosisi ya Kati ya Tanganyika tangu mwaka 1999 kipindi kifupi baada ya kifo cha aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, marehemu Yohana Madinda.

Katika uchaguzi uliomwingiza madarakani alimshinda aliyekuwa Askofu msaidizi wa wakati huo, Donald Mtetemela na kufanya aende kuwa askofu wa Ruaha (Iringa)

Hadi mauti yanamkuta alibakiza miezi kadhaa astaafu kwani ratiba ya kanisa inaonyesha Desemba mwaka huu ingekuwa na uchaguzi
Mungu ailaze mahali pema peponi mtumishi wake huyu

2 comments: for ASKOFU WA ANGLIKANA DODOMA GODFREY MDIMI MHOGOLO AFARIKI DUNIA

  1. Mungu Baba yetu aishie milele akupe makao katika Ufalme wake na awape wepesi wanafamiliya yake ili waikubali kazi ya Mungu asie na mpinzani milele,huwaita wana kwa wakati alioupanga yeye tu.Ni Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe!

    ReplyDelete
  2. Hakika Mungu ni mwaminifu wakati wowote kwetu haswa tukimwomba kwa kumaanisha.

    ReplyDelete