UTATA KUHUSU MAMA ALIYEBADILI DINI NA KUWA MKRISTO
Posted by :
Unknown
on :
Monday, June 2, 2014
0 comments
Meriam na watoto wake kizuizini Sudan
Mumewe mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Suudan kwa kosa la kuasi dini ya kiisilamu, ameambia BBC kuwa hajafahamishwa kuhusu mpango wa kumwachilia mkewe.
Ripoti zilizotolewa Jumamosi ziliarifu kwamba afisa mmoja wa serikali alithibitisha Meriam Ibrahim, aliyejifungua mtoto akiwa kizuizini ataachiliwa katika siku chache zijazo.
Lakini wizara ya mambo ya nchi hiyo imesema kuwa Bi Ibrahim anaweza tu kuachiliwa ikiwa kesi yake ya rufaa itafanikiwa.
Taarifa za hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mwanamke huyo, zimeikera sana jamii ya kimataifa.
Meriam na mumewe ambaye anasema hana habari ikiwa mkewe ataachiliwa
Bi Ibrahim, alilelewa na mama aliyekuwa mkristo , lakini mahakama ilimhukumu kifo ikisema kuwa anapaswa kuwa muisilamu, hiyo ndiyo iliyokuwa dini ya babake.
Alikataa kusilimu na kusema kuwa yeye ni mkristo na hivyo anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuasi dini.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Abdullahi al-Azreg, aliambia BBC Jumamosi kwamba, Bi Ibahim ataachiliwa huru kwani serikali ya Sudan inawapa watu uhuru wa kuabudu na hivyo iko tayari kumlinda.
Mumewe Meriam Daniel Wami, alisema kuwa taarifa za mkewe kuachiliwa ambazo amezisikia kupitia vyombo vya habari, ni kama uvumi tu.
“Hakuna afisaa yeyote wa serikali amewasiliana name. Labda kuna mashauriano kati ya serikali na maafisa wa kigeni , ikiwa ni hivyo taarifa hizo mimi sina,’’ alisema Daniel.
“Mimi nitasubiri tu kesi ya rufaa ambayo mawakili wamewasilisha, na ninatamai kuwa mke wangu ataachiliwa.’’
Waziri wa mambo ya nje alifafanua kuwa Bi Meriam anaweza tu kuwa huru ikiwa mahakama itaamua hivyo katika kesi yake ya rufaa.
(Source:Bbc Swahili)
Saved under :
Habari za Kidini,
Neno la leo
No comments: