Latest News


More

PAPA ATEUA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA DODOMA

Posted by : Unknown on : Friday, November 7, 2014 0 comments
Unknown

Na Frederic M. Gabriel 
wa Globu ya Jamii   
                            
Askofu Beatus Kinyaiya

Hatimaye Baba Mtakatifu Papa Francisco wa kanisa Katoliki duniani amempandisha kutoka Askofu hadi kuwa Askofu Mkuu Askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

Baba Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor tarehe 25 juni, 1989. 

Aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, na kusimikwa/ kuwekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo kuwa Askofu wa jimbo la Mbulu Julai 2, 2006. 

Na leo tarehe Novemba 6, 2014 ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa Jimbo Kuu. 

Askofu Beatus Kinyaiya atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.

No comments:

Leave a Reply