Baadhi ya sample za mashine za kielectronik ambazo zililetwa kwa wanasemina ili waweze kuziona na kuzijua
makampuni mbalimbali yaliyopewa dhamana na TRA ya kuuza mashine hizo za kielectronic walituma wawakilishi wao ili waweze kueleza jinsi zinavyofanya kazi kama huyu dada (jina lake halikupatikana) akielezea
mdau huyu naye toka kwenye kampuni yenye dhamana ya kuuza mashine hizo akielezea matumizi yake
hawa ni wawakilishi wa kampuni ya BMTL nao wakielezea jinsi ya kutumia mashine hizo
wawakilishi wa makampuni yenye dhamana ya kuuza mashine za kielectronic wakiwa tayari kutoa maeleze kwa wana semina
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia ufunguzi wa semina hiyo toka kwa mkuu wa mkoa wa Tanga .Wa kwanza kushoto (mwenye suti nyeusi) ni Tumaini Kichila ambaye alikua mmojawapo wa watoa mada kwenye semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa makini
Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro (mama Minga) akiongozana na mkuu wa mkoa wa Tanga (ambaye alikua mgeni rasmi ) wakiongozana kuingia katika ukumbi wa semina tayari kwa ufunguzi.
Mama Neema Mrema (naibu kamishna idara ya waliopa kodi wakubwa) akiwa na meneja wa mkoa wa Kilimanjario (Mama Minga) wakisubiri kuanza kwa semina nje ya ukumbi.Wengine nyuma yao ni wafanyakazi wa TRA
Idara ya mapato ya walipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwishoni mwa mwezi wa tisa ilifanya semina kwa walipakodi wa kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro , Arusha, Tanga, Manyara na Singida.Nia na madhumuni ya semina hii ilikuwa kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu kodi na kikubwa zaidi mashine ya kielektoniki ya kuweka kumbukumbu ya risiti (EFD) ambayo inatakiwa kutumiwa na walipa kodi wote wanaotoza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kuanzia mwezi wa kumi 2010.Walengwa wa semina hii walikua walipa kodi wakubwa na wakati katika mikoa tajwa .
.Semina hii ilifanyika mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa Lutheran Center.Mgeni wa heshima aliyefungua semina hii ni mkuu wa Mkoa wa Tanga Meja mstaafu Kailembo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Katika nasaha zake mkuu wa mkoa wa Tanga aliwaasa wafanyabisahara kulipa kodi kama ilivyo katika seheria ili kuleta maendeleo katika nchi yetu.Pia aliwataka wafanyakazi wa TRA kufanya kazi kwa moyo na kuongeza ufanisi ili kuongeza mapato ya Tanzania .Aliwapongeza pia wafanyakazi wa TRA kwa kuweza kubuni na kuleta mashine ambayo itasaidia kupunguza kama sio kumaliza mianya ya ukwepaji wa kodi
Pichani juu ni kamishna msaidizi wa Idara ya walipa kodi wakubwa Mama Neema Mrema akiwa pamoja na mwelimishaji wa kodi mkoa wa Arusha ambaye ndiye alikua mshereheshaji (MC) katika semina hiyo akiangalia jinsi wahudhuriaji walivyokua wanajiandikisha mlangoni kabla ya kuingia ukumbi wa semina
No comments: