Latest News


More

Posted by : Unknown on : Friday, February 4, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Ndugu wana blog ni siku nyingine tena ya Ijumaa , kwa wale wafanyakazi wengine wanasema eti wanafunga shule eti kama wanafunzi, kisa ni kwamba wanaenda mapumziko kwa siku mbili Jumamosi na jumapili,
Yote kwa yote ni siku nzuri haswa ukizingatia kesho na kesho kutwa wafanyakazi wanakuwa wanapumzika majumbani kwao au wanakua na mishemishe zao binafsi, na kwa kiasi fulani wanaachana na karaha za kudamka mapema na foleni (haswa kwa wale walioko Dar) kwa wa mikoani mmmh hawana adha kubwa ya kudamka mapema,
Mimi niwatakie kila la heri tu na baraka tele katika week end hii haswa ukizingatia ni week end ambayo mifuko kwa kiasi fulani imenona kwa wale wafanya kazi hivyo angalao mambo si mabaya sana.Ila mwaka nao unakwenda kwa kasi ya ajabu haswa ukizingatia ni juzi juzi tu tulikua tunazungumzia mambo ya Krismas , mara mwaka mpya na sasa tunasubiria Valentine.
Kila la heri wadau na Week end njema tuonane tena wiki ijayo!!!
(Pichani mdau wa blog hii akitoa mada kwenye moja ya semina)