Lakini mahitaji ya watoto hao wachanga yalikuwa makubwa kuliko uwezo wao. Kwa siku watoto hao walitumia jumla ya nepi 50 na chupa 30 za maziwa.Maombi ya msaada toka kwa manispaa yalipokataliwa, Mia alimwambia mumewe waweke pozi na watoto wao na walipiga picha ambayo Mia aliiweka kwenye mtandao wa Facebook.
Ndani ya muda mfupi picha hiyo ilijipatia umaarufu duniani na haikuchukua muda ilimfikia bilionea Oprah Winfrey ambaye alivutiwa na picha hiyo na kuamua kumualika Rozonno na mkewe kwenye shoo yake ya Oprah Winfrey Show.Kwa ukarimu wake, Oprah aliizawadia familia hiyo dola 250,000 za kufanya manunuzi ya mahitaji yao yote wakati wowote wanapotaka kwenye mtandao wa supermarket kubwa Marekani ya Walmart.
Ingawa Rozonno na mkewe walishaoana miaka 11 iliyopita walipokuwa na umri wa miaka 18 na 19, Oprah aliwazadia zawadi ya kwenda fungate (honeymoon) kwenye mojawapo ya hoteli kubwa za mjini Las Vegas.
Nyota wa muziki nyororo wa Marekani, Celine Dion ambaye naye alikuwepo kwenye shoo ya Oprah, aliwapa zawadi ya tiketi ya mstari wa mbele kabisa kwenye shoo yake ya muziki.
Picha waliyopiga pamoja na watoto wao wachanga sita na kisha kuiweka kwenye mtandao wa Facebook imeifanya familia ya Rozonno na mkewe Mia McGhee ya nchini Marekani kujiingizia kiasi cha dola 250,000 zaidi ya Tsh Milioni 325.
(Source Nifahamishe........)