Latest News


More

IBADA YA MWAKA MPYA - USHARIKA WA K.K.K.T MWENGE

Posted by : Unknown on : Thursday, January 3, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : , ,
Siku ya tarehe 1/1/2013 siku ya mwaka mpya waumini mbalimbali wa Kikristo walifanya ibada ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kuingia mwaka mpya 2013.Katika Usharika wa K.K.K.T Mwenge nao walifanya ibada moja iliyoanza saa moja asubuhi mpaka saa tatu na nusu asubuhi

Ibada hii iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiana na Mchungaji Elieza Mchomvu wa Dayosisi ya Pare
Katika Ibada hiyo neno la Mungu lilitolewa na mchungaji Mchomvu ambaye alisisitiza amani na upendo kwa Watanzania wote.Pia alihimiza waumini wa Kikristo kukumbuka kumwabudu Mungu na pia kusaidiana miongoni mwao
Hakika ilikua ni ibada nzuri ambayo mbali na mahubiri ilikua pia na ushiriki wa chakula cha bwana pamoja na shukrwani ya mwaka mpya na maombi maalum


 Pichanijuu na chini baadhi ya waumini wakiwa kwenye ibada hiyo





 Mchungaji wa usharika mchungaji Kaanasia na mchungaji Mchovu wakiimba na kusifu
 Huyu dada aliiongoza kipindi cha sifa.Hakika huyu dada anajua kuimba na ana sauti nzuri ya kuimba.Mungu azidi kumbariki  dada huyu.
 Baadhi ya wanakwaya wa kwaya ya vijana na kwaya ya uinjilisti wakiimba na kusifu kwenye ibada hiyo
 Baadhi ya waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.Anaeonekana mwenye suti nyeusi na nyeupe ni Dr Kitunga mmojawapo wa wazee wa kanisa wa Usharika wa Mwenge


 Mwalimu Kayenze naye akiimba nyimbo za sifa.Bwana Kayenze ni mwalimu kiongozi wa kwaya katika usharika wa Mwenge.Hakika mwalimu huyu ana sauti ya tofauti na kipaji cha aina yake cha uimbaji.Mungu azidi kumbariki



 Hapa mwalimu Kayenze akiimba kwa hisia kali




 Picha ya juu na chini waumini wakishiriki Sakramenti ya meza ya bwana siku ya mwaka mpya



 Baada ya kushiriki sakramenti ya meza ya bwana kulifanyika maombi maalum kwa watu wote.Maombi haya yalifanywa kwa makundi maaluma kama vile vijana, wagonjwa, waliosafiri na kurudi salama kipindi cha sikukuu n.k

No comments:

Leave a Reply