Mwishoni mwa mwaka jana 2012 Kampuni ya Tazara kwa kushirikiana na Clouds FM pamoja na uongozi wa mbuga ya hifadhi ya Selous iliyoko Morogoro ziliandaa safari ya utalii wa ndani kwa treni kutoka Dar kwenda Morogoro kwenye mbuga hiyo na kurudi Dar
Hii ni moja ya mikakati ya kuhamasisha Watanzania kupenda kutembelea mbuga zetu na kuacha dhana inayosemekana swala la utalii ni la wageni kotoka nje ya nchi
Safari hii ilifanyika tarehe 29/12/2012 ambayo ilianza saa 2 asubuhi kutoka kwenye stesheni ya Tazara.Mimi nilipata nafasi ya kuwa mmojawapo wa watalii wandani waliokuwepo kwenye safari hiyo nasi tulienda kama family friend tukiwa familia nne za mme na mke jumla kukiwa watu wanane.Familia hizi ni familia yangu (Kichila) familia ya Bwana Gerald, familia ya bwana Mushi na familia ya bwana Lema.Ni safari iliyokuwa na watalii takriban 450 hivi wakiwa ni wanaume, wanawake pamoja na watoto
Fuatana nami kwenye picha uone jinsi safari yetu ilivyokuwa na mambo tuliyoyaona kwenye safari yetu hiyo
Pichani juu bwana Mushi (mwenye shati la draft) bwana Lema, mke wa Lema aliye nyuma , bwana Gerald na anayeonekana kwa nyuma ni Lilian Kichila na mbele yake yuko mke wa GeraldPichani ni mama James Mushi anayeonekana kufurahia safari pamoja na mke wa Gerald.Hapa ni kabla ya kuanza safari
Bwana Mushi aliye chini na ndani ya treni ni Bwana Kichila na bwana Lema.Hapa ni kabla treni haijaanza safari
Bwana Mushi, Lema, Kichila na kwa mbali anaonekana mke wa Mushi
Bwana Mushi na Bwana Kichila ndani ya kut kruch kruch (treni)
Mandhari ya nje tukiwa safarini kwenda Morogoro
Hii ni baada ya kufika stesheni ya mwisho Huko Morogoro mahali paitwapo Kisaki al maarufu kama maji moto
Baada ya kushuka kwenye treni.Hili ni eneo ambalo ni maarufu kwa maji ya moto.Kuna maji ya moto ambayo unaweza kuuweka mayai na yakaiva kwa muda mfupi sana
Mke wa Gerald akishuka kwenye treni na kwa nyuma anayefuatia ni mke wa Bwana Mushi
Mke wangu Lilian naye hakubaki nyuma . anashuka naye kwenda kushuhudia maji ya moto
Safari ya kuelekea kwenye maji ya moto.Mbele kabisa anayeongoza msafara ni mke wa bwana Mushi, mke wa bwana Lema, mke wa bwana Gerald na mwisho kabisa ni mke wangu Lilian
Baada ya kufika Kisaki tulikuta kikundi cha ngoma za kienyeji , hakika kilikua kinatoa burudani ya uhakika japo hatukujua walikua wanaimba lugha gani
Waimbaji wa kikundi cha ngoma asilia wakiburudisha watalii wa ndani
Hii ndiyo sehemu yenye maji ya moto.Sehemu kubwa hapa kuna chem chem ya maji ya moto ambayo tulitahadharishwa mapema kabla hata ya kushuka kwenye treni kuwa waangalifu kwani pamoja na kuwa na maji ya moto, eneo hili linatitia hivyo usipotembea au kukanyaga kwa uangalifu unaweza kutitia na kuungua na maji ya moto.
Kweli kuna bwana mmoja alikanyaga bila ya uangalifu na akaungua miguu yote miwili hadi kumlazimu kuvua viatu alivyokua amevaa.
Hapa mimi na mke wangu tukijaribu kushika maji ya moto.Aliye mbele ni mke wangu Lilian akishika maji ya moto.Hakika yalikua ya moto na yanaunguza kabisa usipokua mwangalifu.Duh... hakika Mungu ameumba
Hapa karibu family friend yote ikiwa eneo la tukio, toka kushoto Mushi, mkewe, mama Kichila na bwana Gerald.Nyuma ya mke wangu yuko mke wa bwana Lema
Mke wa Mushi na mke wangu wakiwa eneo la maji ya moto
Kwa mbali kruch kruch letu likionekana na watu wakiendelea kupiga picha mbalimbali.Tulikua na karibu crue nzima ya Clouds Fm Redio
Bwana Mushi akijaribu kushika maji ya moto
Hii ni mojawapo ya chem chem kubwa ya maji ya moto eneo hilo
Watu wakirudi kwenda kupumzika baada ya ziara ya kuangalia maji ya moto
Bwana Mushi aliyesimama na mke wa Bwana Gerald, mke wa Lema aliyekaa na mke wa Mushi
Familia nzima (ukiondoa anayepiga Picha.Toka kushoto mke wa Lema, mke wa Gerald, Mushi, Gerald, Lema, mke wa Mushi, na mke wangu Lilian
Familia nzima ukiondoa anayepiga picha bwana Gerald.Toka kushoto mke wa Lema, mke wa Gerald, Mushi, Kichila, Lema, mke wa Mushi na mke wangu Lilian
Hapa bwana Mushi al maarufu kama mwalimu alikua anatoa somo la mahusiano ya mke na mume.hakika bwana Mushi ni mwalimu mzuri sana.
Hii ziara yetu pamoja na utalii tulipata nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali za mahusiano kati ya mume na mke.Hakika ilikua ni mada nzuri sana.Keep it up mwalimu Mushi
Hapa bwana Mushi akiongea kwa msisitizo mada hiyo
Tukijiandaa kuondoka tulipata nafasi tena ya kuchungulia ngoma ya asili, kwa mbaali anaonekana mke wangu naye akifurahia ngoma hiyo
Wadau wakijiandaa kupanda treni tayari kurudi kwenye stesheni ya karibu kwa ajili ya kupata chakula cha mchana
Tukiwa stesheni ya mwisho mahali ambapo tulipumzika kwa muda kwa ajili ya kupata chakula cha mchana, hapa si mbali sana na mahali kwenye chemchem ya maji ya moto.Pichani ni mmojawapo wa staff wa treni ya Tazara akitoa maelezo kwa bwana Mushi na bwana Geradl
Tulipata nafasi pia ya kuongea na dereva wa treni yetu na kuona jinsi treni inavyoendeshwa.Pichani ni dereva ya treni hiyo (jina hatukulipata) akitupa maelezo .Hapa ndiyo shughuli nzima ya kuendesha treni invyoonekana
Hapa ndio kama control room ya treni
Hapa nami nilipata nafasi ya kukaa mahali pa kuendesha treni.. ha ha haaa hakika waswahili wanasema tembea uone mengi
Wadau Gerald , Mushi na mdau mwingine wakifuatilia maelezo ya uendeshaji wa treni
Bwana Lema akiwa mbele kabisa ya treni hiyo
Mwisho wa safari yetu tulifika stesheni ya Tazara takriban saa tatu za usiku siku hiyo hiyo
Hakika ilikua ni safari nzuri japo ilikua na mapungufu mbalimbali ambayo waandaaji wakiyafanyia marekebisho hayamkini Watanzania watahamasika kufanya utalii wa ndani kipindi kijacho
Baadhi ya mapungufu makubwa yalioonekana ni kama vile
1.Abiria kukosa chakula cha mchana baada ya kuwa na utaratibu mbovu wa kugawa chakula hicho
2.Kuwepo na party ya Clouds ndani ya treni.Hii ilileta usumbufu kwa kuwa ilikua ni kati ya behewa la cafteria na mabehewa mengine hivyo kuleta usumbufu wa kupita toka behewa hilo kwenda kwenye behewa la chakula na vinywaji.Kipindi kijacho kama kutakuwa na party basi ni bora wawe kwenye behewa la mwisho kabisa ili kuondoa usumbufu
3.Mwisho ni kutoona wanyama kama ilivyokuwa dhumuni la safari nzima.Wanyama wengi huwa wanakimbia pale treni inapopita kwa sababu ya kelele.Hivyo wanyama walioonekana ni kama tembo, digi digi, pundamilia, ngiri, swala tena kwa mbaali sana
Hivyo ushauri wangu ni kuwa wakifanya tena safari kama hivyo waandae mabasi ili watalii wakifika stesheni ya mwisho ya Kisaki washuke na kupanda mabasi au magari mengine yatakayowapeleka mbugani ili waweze kuwaona wanyama kwa karibu na wengi zaidi tofauti na kuwaona wakiwa njiani, na hii ndiyo italeta maana ya utalii wa kuona wanyama.Otherwise itakuwa ni utalii wa kwenda kuona maji ya moto
No comments: