Waumini wa kusini (mikoa ya Lindi na Mtwara) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) hatimaye wamepata Dayosisi yao mpya pamoja na askofu wao wa kwanza
Askofu
wa Dayosisi hiyo ya kusini ni Askofu Lucas Mbedule ambaye wiki iliyopita alisimikwa rasmi kuiongoza Dayosisi hiyo
Ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya waumini na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Pinda iliambatana na kuizinduia rasmi Dayosisi hiyo.Ibada hiyo iliongozwa na mkuu wa kanisa la K.K.K.T Dr. Alex Gerhaz Malasusa pamoja na maaskofu mbalimbali wa kanisa hilo.
Picha ya juu ikimwonyesha Askofu Mbedule mara baada ya kusimikwa rasmi kuiongoza Dayosisi hiyo ya Kusini
Ibada hiyo ilifanyika katika kanisa la Kilutheri la mjini Mtwara Mei 26, 2013
Picha ya juu ikimwonyesha Waziri mkuu Mizengo Pinda (ambaye alikuwa mgeni rasmi) akimkabidhi
zawadi ya picha, Askofu wa kwanza wa Dayosisi ya Kusini Mashariki, Askofu
Lucas
Mbedule .
Kushoto ni Mkuu wa K.K.K.T nchini, Askofu Dk Alex Gerhaz Malasusa na (kushoto)
ni Mchungaji wa Dayosisi hiyo, Y. Y. Ngwema.
(Picha kwa hisani ya Robert Okanda)
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: