ADUI YAKO
NI NANI?
Ingawa tunasema Mkristo anatakiwa aishi kwa amani na watu wote
(soma Warumi: 12:18), maana ya kuunganika kwake na Yesu Kristo ni kwamba watu wengine watamchukia.
Kwa hiyo Mkristo huyu atakuwa na maadui wengi.Na ujue kwamba adui yoyote
yule wa Mkristo ni adui wa Mungu, na maadui wa Mungu ni maadui wa Mkristo vile
vile.(Kut.23: 22;Zab 37: 20;55:2-3;Mt 10:22,36)
Hata hivyo tunaaswa na Yesu Kristo kwamba Mkristo anapaswa kuwapenda adui zake na kuwatendea mema watu wanaomchukia
(Mt 5:44;Lk 6:27)
Biblia inaeleza habari za maadui wengine kuliko wanadamu wenzetu,
mfano ni
Shetani,maadui na mamlaka mbaya ya kiroho.
Lakini Kristo alishinda uadui wote kwa njia ya kufa na kufufuka kwake,na siku ya ushindi
wake wa mwisho atawaangamiza maadui wote mpaka milele (Mt 13:39;Lk 10:18; Kol 2:15)
(Kichila Tumaini S - 2013)
No comments: