Latest News


More

MSTAHIKI MEYA WA ILALA AONGOZA TAMASHA KUBWA LA UJENZI WA KANISA LA K.K.K.T SEGEREA

Posted by : Unknown on : Monday, May 27, 2013 0 comments
Unknown
 Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala ndugu Jerry Silaa jana jumapili iliyopita aliongoza tamasha kubwa la uimbaji ambalo lilikua na lengo la   kupata fedha za ujenzi wa kanisa  la K.K.K.T Usharika wa Segerea

Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam siku ya jumapili tarehe 26/05/2013 kuanzia saa 8.00 mchana na kuhudhuria na maelfu ya watu

Katika tamasha hilo lilihudhuriwa na waimbaji wengi maarufu kama vile Solomon Mukubwa kutoka Kenya, Martha Mwaipaja, Brother Joshua Mlelwa, Kwaya kuu ya K.K.K.T Usharika wa Magomeni, AIC Chang'ombe, Ambwene Mwasongwe, Edson Masabwite, Trinity Band , Kwaya ya Lulu ya Mtoni , kwaya ya Umoja ya K.K.K.T Usharika wa Segerea na wengine wengi.


 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza harambee hiyo
 Watu mbalimbali walihudhuria harambee hiyo kama wanavyoonekana juu na chini

 Waimbaji wa sifa wa Usharika wa Segerea wakiimba kwenye harambee hiyo .Pembeni ni Mc wa harambee hiyo dada Ritha Chiwalo
 Sehemu ya wageni waliokaa meza kuu.Kutoka kushoto mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ndugu Samson Zanny, Mchungaji Kadiva (ambaye alimwakilisha baba Askofu Malasusa), mchungaji Kipingu (Mchungaji kiongozi wa Usharika)akiwa na mke wake na wachungaji wengine walioalikwa kwenye harambee hiyo
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa kanisa wakiwepo wachungaji wakiwa kwenye tamasha hilo lililoambatana na harambee ya ujenzi wa kanisa

 Juu na chini waumini waliohudhuria tamasha hilo katika ukumbi wa Diamond Jubilee

 Mwimbaji wa kimataifa kutoka Kenya Solomon Mukubwa akiimba jukwaani siku hiyo ya jana.Mwimbaji huyo alisindikizwa na waimbaji wa sifa kutoka Usharika wa Segerea
 Mwimbaji Martha Mwaipaja akiimba jukwaani huku akisindikizwa na Solomon Mukubwa na Mc wa harambee hiyo Ritha Chiwalo
 Meza kuu akiwepo mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ndugu Samson Zanny, Mchungaji Kadiva na mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa wakifuatilia tamasha hilo
 Mchungaji wa Usharika wa Segerea Mchungaji Kipingu akiwashukuru watu waliohudhuria tamasha hilo
 Mchungaji Ernest Kadiva (Naibu katibu mkuu Utawala na utumishi) wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani  akizungumza machache.Mchungaji  Kadiva alimwakilisha askofu wa Dayosisi Dr Alex Gerhaz Malasusa ambaye yuko safarini.Pe,beni yake ni mchungaji wa usharika wa Segerea mchungaji Kipingu
 Mgeni mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa rasmi akizungumza  machache kabla ya kuanza harambee hiyo hapo jana

Mwenyekiti wa ujenzi ndugu Alex Molel akichangia katika ujenzi huo.Ndugu Mollel alichangia shilingi milioni moja  kwenye harambee hiyo.
 Wageni mbalimbali wakiahidi mbele ya mgeni rasmi siku hiyo ya jana

 Kamishna mstaafu S.Mwanguko na mke wake wakichangia katika ujenzi huo
 Katibu wa baraza Prof Majule na mkewe wakichangia katika harambee hiyo.Prof Majule na mke wake walichangia Dola 2000
 Emmanuel Kwayu (papaa aka Mutu ya Mungu) ,mwenyekiti Zanny, mwimbaji wa kimataifa Solomon Mukubwa, Mc wa tamasha hilo Ritha Chuwalo, Noel Tenga na Mdau wakiwa kwenye picha ya pamoja

 Sehemu ya meza kuu.Mwenyekiti wa ujenzi Alex Mollel, Katibu wa baraza Prof Amos Majule, Mwenyekiti wa kamati ya tamasha bwana Zanny, naibu katibu mkuu utumishi na utawala Mchungaji Kadiva na mgeni rasmi wakifuatilia tamasha hilo
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bwana Zanny akiteta jambo na mgeni rasmi.Katikati ni mchungaji Kadiva ambaye alimwakilisha askofu wa Dayosisi Dr Malasusa

 Mchungaji Kadiva akiongea machache.Katikati ni Mgeni rasmi (mstahiki Meya wa Ilala) Silaa, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bwana Zanny na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Segerea Mchungaji Kipingu
 Wanakwaya wa kwaya ya AIC Chang'ombe wakiimba jukwaani
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiwa ameshika picha ya mgeni rasmi.Picha hiyo Bwana Zanny aliinunua kwa shilingi milioni 5.5

Dr Kakiko katibu wa Ujenzi akichangia katika ujenzi huo.Dr Kakiko alichangia shilingi milioni moja.
 Waimbaji maarufu wa kwaya ya Lulu ya Mtoni Dar es salaam wakiimba jukwaani wimbo wao maarufu wa Lulu
 Pichani Mstahiki meya akiwa na Samwel Samson  (mtoto wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi)  pamoja na baba yake .Mtoto huyo alichangia shilingi laki moja ya ujenzi wa kanisa hilo.Mr Samson


 Pamoja na tamasha na harambee hiyo ya Ujenzi pia kulikua na tendo la kuzindua kanda ya Video ya kwaya ya Umoja ya  kanisa la Segerea.Pichani juu Mstahiki Meya akizindua kanda hiyo
Pichani Msatahiki meya Jerry Silaa akiizindua kanda hiyo.Pembeni ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi  ya harambee hiyo Ndugu Samson  Zanny

 Kulia bwana Emmanuel Kwayu (mratibu wa waimbaji) , Peter Munuo (katibu wa tamasha) wakifuatilia mahesabu na mgeni rasmi

Picha ya wanakamati wote mara baada ya tamasha hilo la ujenzi wa kanisa
Jumla ya shilingi zaidi ya milioni73 zilipatikana zikiwa kama  fedha taslim na ahadi takriban shilingi milioni 83.Pesa hizo zilipatikana pia  kupitia vitu mbalimbali vilivyonadiwa siku hiyo ya tamasha

SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA!!

No comments:

Leave a Reply