OMBENI KATIKA JINA LA BWANA YESU
KRISTO
MAOMBI NI NINI?
Maombi ni hali ya mwanadamu kuwa na mawasiliano na Mungu
Maombi kwa mwamini ni ibada tosha bila kujali anafanya hayo
maombi wapi na kwa muda gani
Maombi ni tendo la imani kwa mwamini
Maombi ni njia ambayo mwamini anaitumia kuvumbua vitu
ambavyo havionekani; katika ulimwengu wa giza
Maombi ni hali ya mwamini kumtegemea Mungu
Maombi ni maisha ya mwamini
Muda wa maombi ni muda wa kuwekeza , ni kipindi cha kupanda
Mfano Yesu Kristo alitumia muda wake mwingi na wa kutosha
kuomba
“Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda
zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko"….Marko 1:35
Pia waweza kusoma Luka 6: 12 na Luka 22: 40 – 45
Maisha ya maombi hubadilisha sura ya nje ya mtu
Mungu anajibu maombi;ndio maana alituagiza tuombe (Mathayo
7:7-11)
Ø
Maombi ni silaha kubwa sana kwa mwamini;kuomba
kunaleta mafanikio makubwa sana kwa waaminio
Ø
Mungu anasemaje
kuhusu maombi ? Yohana 16:24;
“Hata sasa hamkuomba neon kwa jina
langu;ombeni nanyi mtapata,furaha yangu iwe timilifu”
Hii ina maana kwamba Mungu furaha yake ni
kujibu maombi yetu, ila hatujibiwi kwa sababu hatuombi vizuri, twaomba kwa
faida yetu wenyewe
Mungu anajibu maombi hivyo kwa mwamini
isipite siku bila ya kuomba
Kumbuka maombi ya Ibrahim yalimwokoa Nduguye
Lutu pale ambapo Mungu alivyotaka kuiangamiza Sodoma na Gomora
Lakini;
Kuomba kunaambatana na kusoma neno la Mungu wakati wote
Maombi ni maisha ya mwamini ya kila siku (Zaburi 55: 16 –
17)
Maombi hayana saa, siku au siku maalum, ila Mungu anasikia
maombi yetu saa, na wakati wowote tumwombapo
1 Yohana 5: 14-15)
KUMBUKA;
Maombi huumba hivyo tusiombe maombi mabaya
Usimwombee mtu mabaya kwa kua amekufanyia jambo baya.Mwombee
mambo mazuri siku zote
Maombi mabaya majibu yake yanatoka na kujibiwa toka katika
ufalme wa giza (kwa shetani) na wala sio kwa Mungu
Mungu anasema mwombee adui yako mema na wala sio mabaya
Wengine wanaomba maombi ya kichawi, mfano baba mdhoofishe
kabisa yule adui yangu, mtupe kuzimu…hayo ni maombi ya kichawi.Kama mwamini wa
kweli huwezi kuomba maombi kama hayo
VIZUIZI VYA MAOMBI
1. Mtazamo mbaya wa mwombaji
Mtazamo mbaya ni sumu ya maombi ya mwamini
kujibiwa
Uwe positive katika maombi yako
2. Hofu huzuia maombi
2 Tim 1 – 7
·
Mtu anayesita sita katika njia yake hawezi
kupokea toba kwa bwana
·
Jinsi Mungu alivyo ndivyo nasi tulivyo kuwa
Positive katika kile tuombacho
·
Imani na hofu ni maadui wawili ambao hawakai
pamoja hata siku moja
·
Tafsiri ya hofu siku zote ni kumwambia Mungu
hawezi kujibu maombi yako
·
Ukimtegemea Mungu hofu yote hupotea
·
Mtu mwenye hofu maombi yake hayajibiwi (Yakobo 1: 5 – 7)
3. Uasi (dhambi)
Aina yoyote ya kutomtii Mungu ni dhambi
Dhambi ni matokeo ya kuasi au kutokutii
Yakobo 1: 21 -22, Isaya 59:1 – 3, Mithali
28: 9 na Zab 66: 18 – 29
4. Mahusiano mabaya ya kifamilia
1 Petro 3:7
“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu
kwa akili, na kumpa mke heshima , kama chombo kisicho na nguvu;na kama warithi
pamoja wa neema ya uzima,kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"
5. Uchungu na kutokusamehe
Hiki nacho ni kikwazo cha mwamini
kutokujibiwa maombi yetu.Unapokosewa na mtu basi samehe ili na wewe usamehewe na Mungu
NAWATAKIA WEEK END NJEMA!!
Mungu awabariki sana!
Kichila Tumaini S
No comments: