Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Segerea mchungaji Noah Kipingu pamoja na Kamati Mkakati wa Tamasha wanapenda kukukaribisha kwenye tamasha kubwa la kihistoria litakalofanyika siku ya jumapili tarehe 26/05/2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee la kuchangia ujenzi wa kanisa la Usharika wa Segerea
Picha ya juu inaonyesha jinsi nyumba hiyo ya ibada itakavyoonekana mara baada ya ujenzi wake kukamilika
Picha ya juu inaonyesha ujenzi wa kanisa hilo ulikofikia kwa sasa hivi
Katika tamasha hilo kutakuwa na waimbaji mbalimbali watakaohudumu ambao ni pamoja na;
1.Solomon Mukubwa kutoka Kenya
2.Brother Joshua Mlelwa
3.Martha Mwaipaja
4.Ambwene Mwasongwe
5 Joshua Makondeko
6.Kwaya maarufu ya Lulu Mtoni
7.Kwaya ya AIC Chang'ombe
Pamoja na kwaya ya umoja Segerea na Segerea Praise Team
Kiingilio katika tamasha hilo Tsh 10,000 kwa viti vya kawaida na Tsh 20,000 VIP (wageni maalum).Ukitoa kiingilio itakuwa ni sehemu yako ya kuchangia ujenzi huo wa nyumba ya Bwana
Ticket zinapatikana sehemu mbalimbali kama vile kwenye makanisa ya K.K.K.T Segerea, Magomeni, Kariakoo, Azania Front, Kijitonyama,Msasani na Kinondoni
WOTE MNAKARIBISHWA
No comments: