Watu wane wamekufa na 13 kujeruhiwa katika mkanyagano ndani ya
kanisa la kiavengalisti nchini Ghana.
Ajali hiyo ilitokea pale waumini walipoania kufikia maji matakatifu katika
tawi la kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) katika mji mkuu,
Accra.Ripoti zinasema maelfu ya watu walikuwa wamekwenda kanisani humo.
Kanisa hilo liloanzishwa na kasisi wa Nigeria, TB Joshua, ambaye anasema yeye ni mtume.
No comments: