Jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge ilifanyika semina yenye kichwa kinachosema " Mtazamo wa Mungu juu ya Familia"
Semina hiyo ambayo inafundishwa na mwalimu Kavishe (pichani juu), ni ya mwezi mmoja ilianza jumapili tarehe 2/06/2013 na itandelea kwa muda mwa mwezi mmoja
Katika somo la siku ya kwanza mwalimu Kavishe aligawa somo hilo katika vipengele vikuu vifuatavyo;
Kwanza:Mungu ndiye mwanzilishi wa familia hapa duniani
Shetani yuko katika kupambana na vitu alivyoanzisha Mungu ndiyo maana familia nyingi zinapita kwenye changamoto za maisha
Hivyo unavyoingia kwenye familia jipange sawasawa kupambana na hila za shetani
Ombea familia ukimsihi Mungu aendelee kulinda familia yako
Pili: Mungu ana malengo na familia zetu (Mwanzo 1:26)
"Wakatawale samaki ........."
Mungu ana malengo na familia na lengo lake kuu ni kutawala vitu vyote ambavyo Mungu ameviumba.Na wao watawaliwe na Mungu
Jipange vizuri kuhakikisha kuwa unatimiza malengo ya Mungu juu ya familia yako
Tatu:Mungu ndiye mwanzilishi wa mahusiano kati ya mtu mke na mtu mme (Mwanzo 1:27)
Mungu aliumba mwanamke na mwanaume akijua kuwa kwa kufanya hivyo atapata familia .Ndoa ni ya jinsia mbili yaani mtu mke na mtu mme
Mungu anachukia watu waliokwisha oana kuachana kwani nia na madhumuni yake kuanzisha mahusiani ni watu wadumu kwenye uhusiano huo.
Nne:Mungu alitengeneza mazingira ili mwanadamu aishi vizuri (Mwanzo 2:15)
Mungu aliumba mazingira kwa siku tano na siku ya sita akaumba mwanadamu ili akae kwenye mazingira mazuri
Mazingira yako yakiharibika kila utakalofanya kitaharibika
Tengeneza mazingira yako ili ufanikiwe katika maisha yako
Mazingira yako yawe ya amani, furaha, utulivu - utaishi vizuri, na unaweza kusali na hata kufanya kazi vyema
Shetani anachofanya kila siku ni kuharibu mazingira yako yawe si ya amani, si ya upendo, ni ya dhiki ili akamilishe kusudi lake hapa duniani.
Ombea mazingira yako yawe mazuri
Tano: Mungu anataka uwe na mahusiano ya karibu na familia yako (Mwanzo 3:8)
Kwa nini baba au mama hataki kuwa karibu na familia yake?
Kama Mungu mwenyewe alikua na mda wa kukaa na Adam na Eva na akaweza kufuatilia maendeleo yao, kwa nini wewe unashindwa kuwa karibu na familia yako na kufuatilia maendeleo yake?
Mwalimu alimalizia kwa kusema lazima Mkiristo uwe na muda wa kukaa na familia, muda wa kusali na muda wa kufanya kazi.Na lazima vyote vibalance
Pamoja na ibada ya semina la nenola Mungu baadhi ya waumini walimtolea Mungu shukrwani mbalimbali.Pichani juu mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi akiongoza maombi hayo
Waumini waliomtolea Mungu shukrani zao
Pamoja na mambo mengine Kwaya ya vijana walionyesha baadhi ya nyimbo waliziziandaa kwenda kuimba kwenye tamasha lililofanyika katika Usharika wa Wazo Hill.Pichani juu mchungaji Kaanasia Msangi akiteta jambo na mzee wa kanisa mzee Mushi wakati wakijiandaa kuwaangalia kwaya ya vijana
Waumini na viongozi walioongoza ibada hiyo pamoja na mzee wa kanisa mzee Nyaki wakisubiri kuangalia kwaya ya vijana
Kwaya ya vijana ikiimba .Kwaya hii inaongozwa na mwalimu Kayesi
Waimbaji wa kwaya ya Vijana wakiimba wimbo wa utamaduni.Wimbo huu ulikua wa asili ya Kimasai
No comments: