JE
UNAWAJUA WAYAHUDI?
Jina la Wayahudi halikutumiwa katika Agano la
Kale
kabla ya kugawanywa ufalme wa Israel.Baada ya kufa kwake Sulemani ufalme uligawanywa katika sehemu mbili,
yaani sehemu ya Kaskazini iliyoitwa Israel na sehemu ya Kusini iliyoitwa Yuda.
Ingawa watu wa ufalme wa kusini walikuwa Waisraeli kwa damu
(kwa sababu wao pia walikuwa wazao wa Yakobo, au
Israeli),waliitwa Wayuda ili kuwatofautisha na watu wa ufalme wa Kaskazini.Baadaye waliitwa Wayahudi
(Yeremia 34:9)
Baadaye falme zote mbili ziliangamizwa, na watu
wake walipelekwa kifungoni katika nchi za kigeni.Halafu wazao wa wafungwa wale
waliporuhusiwa kurudi katika nchi yao ya Israel, wengi wao waliporudi walikuwa wale
wa ufalme wa kusini, yaani Wayahudi.
Wakati ule jina la
Wayahudi lilitumiwa kila mahali na kwa wote walioishi katika nchi yao ya zamani wakati huo,
pasipo kutaja kabila la asili yao.Kwa maneno mengine
,jina lile lilitumiwa kwa Waisrael wote.(Ezra 6:7;Neh 6:6;Dan 3:8)
(Mt 2:2;Yn 1:19;2Kor 11:22; 1 Kor 9:20;Flp 3:5;Rum 1:16
(Imeandaliwa na Kichila - 2003)
No comments: