WAAMINI wa Kanisa Katoliki nchini wametakiwa kuacha tabia ya kutafuta
fedha kwa njia zisizo halali na kuzipeleka nyumbani kwa matumizi ya
familia kwa sababu fedha hizo hazitakuwa na baraka kwa watoto wao.
Paroko
Msaidizi wa Parokia ya Kurasini, Padri Marcel Mukadi alisema suala la
kutafuta fedha kwa njia zisizo halali ikiwemo kuwa na ndimi mbili ni
kuharibu maisha yao.
Akitoa Mahubiri wakati wa ibada ya misa takatifu
kwa Wanahija wa Kanda ya Mtakatifu Martin de Pores iliyopo katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus Kurasini waliofanya hija katika
Kituo cha Mbagala Msalabani, Padri Mukadi alisema:
“Angalieni maisha
ya undumilakuwili si mazuri utapenda kumfurahisha mmoja zaidi ya
mwingine na kuwa nafsi yao itakuwa ikifadhaika kwa kufanya vitendo hivyo
na kamwe hautakuwa na furaha kuwa na majukumu mawili mawili kwa wakati
mmoja kunaharibu maisha maana ndimi mbili hazikai pamoja”.
Aliendelea
kusema wanahija hao waache kuwa vitendo vya ndimi mbili kwa kuwa
vinasababisha waamini washindwe kumuabudu Mungu kwa wakati na kwa njia
iliyo nyoofu kutokana na kushika mambo mawili ambayo ni ya Mungu na ya
Shetani.
Alisema waamini wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya
ushirikina kutafuta fedha ili kuwa na maisha mazuri kitu ambacho ni
hatari kwa sababu fedha watakazozipata zitakuwa ni za majuto hapo
baadaye mara maisha yao yatakapoharibika.
Padri Marcel alisema fedha
wanazozipata kwa njia hiyo ya ushirikina huziharibu familia zao hasa
watoto ambao baadaye wanaweza kupata madhara bila ya wao kujua.
Paroko
huyo alitoa onyo kwa Waamini hao kuacha tabia ya kupeleka fedha
nyumbani kwa matumizi ya familia zilizopatikana kwa njia isiyokuwa
halali ili kuwanusuru watoto wasio na hatia.
“Unaenda kwa waganga wa
kienyeji unapata fedha na kuzirudisha nyumbani unafikiri mwisho wake ni
nini ni kuwa watoto mazezeta halafu unalalamika hebu fikiria wewe
unakula rushwa kwa ajili ya kitu fulani kizuri unafikiri rushwa itajenga
maisha yako kama umechukua rushwa basi tumia wewe mwenyewe na si
kuipeleka nyumbani kwa Watoto”,alisema Padri Marcel.
Hata hivyo
alifahamisha kwamba vitendo vya utoaji mimba navyo ni hatari kwa maisha
yao kwa sababu vitakuwa mwiba punde watakapozaa watoto wengine kutokana
na watoto waliowapotezea maisha kwa kutoa mimba kuwalilia.
Padri
Marcel alisema watoto watakaozaliwa na mtu aliyetoa mimba hawatakuwa na
maisha mazuri hivyo Yesu waliyemfuata katika kituo hicho cha hija
Mbagala awe kidole cha kuwaonesha mguu wao ukae wapi kwa kutawala maisha
katika maisha yao yao huku Roho Mtakatifu akiwa Kiongozi wao kwa kuwa
alisema ‘waonje ya kuwa bwana ni mwema.
Akitoa mfano wa Mtakatifu
Paulo alivyomlilia Mungu kutokana na majivuno yake Padri Marcel alisema
mtume huyo alikuwa na afya iliyozorota hana uwezo wa kuhubiri Injili
licha kuwa na elimu ya dini kutokana na udhaifu huo alimlilia Mungu ili
awe na uwezo huo wa kuhubiri lakini Mungu alimwambia neema yake inatosha
hivyo aliwataka waamini hao kumlilia Mungu ili aweze kuwapatia neema
katika maisha yao.
Alisema wapo wahubiri katika Agano la kale
waliojaliwa uwezo wa kuhubiri habari njema waliokuwa wakimcheka Mtume
Paulo kwa afya aliyokuwa nayo kwa sababu Mungu alimpa uwezo.
“Paulo
alikuwa na afya iliyozorota alikuwa Mfarisayo na alikuwa na elimu ya
dini lakini hakuwa na kipaji katika kuhubiri hivyo alisema nilimuomba
Mungu kwa ajili ya majivuno yangu nisije nikajivuna kupita kiasi naye
akaniambia neema yangu yatosha hivyo tujifunze kutokana na Paulo
alivyowekewa mwiba mwilini mwake asije kuwa na majivuno”.
“Tujifunze
kuwa Mungu ana uwezo wa kufanya chochote ndani yetu anaweza kukupa gari
na akaliharibu kwa ajali hivyo leo Mungu anasema neema yake inatutosha
ni kwamba hakuna kitu kinachotendeka ndani yetu bila ya sababu bali
tuseme neema yake yatutosha tunapokuwa katika majaribu yake tumrudie
yeye ndiye kila kitu katika maisha yetu”,alisema Padri Marcel.
Kabla
ya Ibada hiyo ya misa takatifu, Padri Marcel alitoa semina kwa wanahija
hao kuhusu Mama Bikira Maria na kueleza kwamba hija ni safari ya kwenda
kumuomba Mungu na kupata neema ambayo kila mtu aliyekwenda kuhiji
anakuwa na lengo lake binafsi la kuomba.
Padri Marcel aliwataka
Wanahija hao kuangalia msalaba huo na kuona uwepo wa Mama Bikira Maria
chini yake kama maandiko yanavyosema wakati Yesu Kristo alipokuwa
msalabani kwa kumwambia Yohane mtoto tazama Mama yako na Mwanamke tazama
mwanao hivyo wamchukue Bikira Maria na kwenda naye nyumbani mwao.
Alibainisha
kama ilivyokuwa maana ya hija ni safari lakini umbali wa wao kufika
katika kituo hicho cha hija ni mfupi hivyo lengo lao ni kuwa na Yesu
ndiyo maana wamefika hapo chini ya Msalaba hivyo kama wataomba kwa imani
kupitia mama Bikira Maria aliye chini ya Msalaba huo watafanikiwa.
Alidokeza
Mama Bikira Maria alikuja duniani ili kuleta uhai baada ya mwanadamu
kuleta kifo ndiyo maana Mungu alimuandaa ili amzae Emanuel na hivyo
kuweka agano jipya kwake na kuwataka Waamini hao kumpelekea shida zao
ili aweze kuwasaidia kwa kuzipeleka kwa mwanae Yesu Kristo kama
alivyofanya katika harusi ya Kana walivyoishiwa divai.
Kituo cha Hija
cha Mbagala kilianza kufahamika kwenye Jubilei kuu ya miaka 2000 baada
ya kuzaliwa Kristo na kuteuliwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam
Polycarp Kardinali Pengo kuwa ni kituo cha hija kutokana na Msalaba
uliosimikwa na Padri Maurus Hartmann kabla ya vita ya kwanza ya Dunia
mwaka 1914-1918 ulioonesha ni eneo la kuwazika wakristo.
Baada ya
kutangazwa kuwa ni kituo cha hija Wanaparokia wa Kituo cha Kiroho cha
Mbagala hasa waliokuwa wakiishi karibu na Kituo hicho walihamasika na
kuanza kusafisha eneo hilo la Msalaba na kulizungushia ukuta ambapo
baada ya Jubilei kuu watu wamekuwa wakienda kusali.
Msalaba huo
ulitokana na umuhimu wa kuwepo kwa mahali pa kuzikia watu baada ya Padri
Maurus kununua eneo hilo la Mbagala mwaka 1901 baada ya Kurasini,eneo
la Kurasini kuonekana halifai kwa kilimo na hivyo kuwahamishia Vijana
hao waliokuwa wakitunzwa na Kanisa la Kurasini baada ya kukombolewa
kwenye biashara ya utumwa.
Aidha hata wale waliokuwa yatima
walitunzwa katika eneo hilo la Mbagala ambapo makaburi hayo yalikuwepo
hadi mwaka 1971 na kuharibiwa na watu waliokuwa wakitafuta viwanja
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)

No comments: