Rio de Janeiro, Brazil
Papa Francis amezuru eneo hatari lenye uhalifu mwingi mjini humu na kusema vijana ndio chachu ya mabadiliko na maendeleo ya imani katika Kanisa Katoliki duniani.
Katika ziara yake kwenye makazi ya watu maskini na
uhalifu mwingi uliokithiri ya Varginha, Papa Francis alisema kuwa
vijana hawana budi kuingia mitaani kuhubiri Injili bila hofu, woga na
kueleza kuwa kanisa lisilowafikia wengi hugeuka chama cha kiraia au cha
kibinadamu.
“Mkifanya hivyo, sina shaka majimbo yenu yatabadilika pia, imani itakuwa na mizizi na neno la Mungu litawafikia wengi.
“Msifanye mzaha, fanyeni fujo katika kuhubiri,”
alisema Papa Francis katika hotuba kwenye ufunguzi wa Siku ya Vijana
Duniani kwenye ufukwe maarufu wa Copacabana uliojaa maji, matope
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Ninataka kuona fujo majimboni mwenu!” alisema kwa Kispaniola na kuongeza: “Ninataka kuona kanisa likiwa karibu na watu.
“Ninataka kuona mnaachana na mazoea kwamba
uinjilishaji ni kazi ya makasisi, kanisa la kujifungia ndani ya parokia
zenu, shule au zahanati zenu. Ninataka mtoke nje!”

No comments: