Latest News


More

WAPENI WATOTO SADAKA BORA NA SI BORA SADAKA

Posted by : Unknown on : Monday, July 1, 2013 0 comments
Unknown

Mwalimu Kawiche akifundisha kwenye semina jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge aliwaasa wazazi kuwaruhusu watoto wao kwende ibadani.Pia aliwaasa waache tabia ya kuwapa watoto mabaki ya fedha kama sadaka za kupeleka kanisani
Alisema mara nyingi wazazi huwa wanawatuma watoto kununua mahitaji kama sukari, mchele, mikate nk. kisha pesa inayobaki huwapa watoto wao wapeleke kanisani

Mtoto naye anaangalia vitu anavyopenda anavyovipa kipaumbele kama pipi, biscuit nk na kununua kwanza kisha mabaki ya pesa ndiyo hupeleka kanisani hivyo hukuta anapeleka shilingi mia au hamsini au mara nyingine kutopeleka kabisa

Watoto Evelyn Kichila na Omega Msangi wakiwa kanisani Usharika wa Mwenge

Mwalimu Kawiche aliwaasa wazazi kuwafundisha watoto kumtolea Mungu sadaka bora na wala si bora sadaka na kwa kuwafundisha hivyo watakua wakijua kwamba Mungu anatakiwa apewe sadaka nzuri na wala si mabaki au senti zinazobaki baada ya kufanya mahitaji yetu
 Wanafunzi wa Sunday School wakiwa ibadani Usharika wa Mwenge jumapili hii
 Waaalimu wakiwafundisha watoto wa Sunday School kwenye Usharika wa Mwenge jumapili hii

No comments:

Leave a Reply