Ibada hiyo imeandaliwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika huo Mchungaji ElionaKimaro,ofisi yake wakishirikiana na baraza la wazee na washarika wa Kariakoo
Ibada hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi itafanyika katika kijiji cha Chasimba na itaongozwa na mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) Dr. Alex Malasusa na mgeni rasmi atakuwa makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bilal pamoja na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Ibada hiyo itaanza saa mbili kamili asubuhi na kuendelea.Kwaya zitakazohudumu katika ibada hiyo ni kwaya kuu ya Usharika wa Kariakoo pamoja na kwaya ya tarumbeta .
Neno kuu litakaloongoza:
"Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kwa kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.Yakobo akaondoka asubuhi na mapema,akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa " ...(Mwanzo 28:16-19)
"MUNGU AWABARIKI"
No comments: