Juma la missioni limezinduliwa jumapili hii katika usharika wa Sinza wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (K.K.K.T).Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mkuu wa kanisa la K.K.K.T Askofu Dr Alex Malasusa na viongozi mbalimbali wa dayosisi hiyo.Pia ibada hiyo ilihudhuriwa na wachungaji mbalimbali wa sharika za jimbo la Kaskazini.
Upandaji wa mti wa kumbukumbu ya juma la misioni ulipandwa na askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri la Bavaria ujerumani askofu Heinrich Bedford Strohm
Mama Akanasia Lema akimsaidia askofu Heinrich Bedford wa Bavaria Ujerumani kupanda mti wa kumbukumbu
Mama Akanasia Lema akisaidia kupanda mti wa kumbukumbu ya juma la missioni.Pembeni yake aliyeshika chepe ni askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri Bavaria Ujerumani askofu Heinrich Bedford Strohm
Mkuu wa kanisa akiingia kwenye ibada baada ya kuzindua kanisa la Usharika wa Sinza na kuzindua juma la missioni
Pichani juu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Dr Alex Malasusa akizungumza wakati wa ufunguzi wa juma la missioni katika Usharika w a Sinza.Aliyeshika mti ni mama Akanasia Lema wa Usharika wa Sinza
No comments: