Latest News


More

Mchungaji azuia Wanawake kwenda Kanisani na wigi

Posted by : Unknown on : Sunday, August 25, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Texas – Marekani
Mchungaji wa kanisa la Resurrecting Faith la mjini Texas Marekani amepiga marufuku waumini wake kuvaa nywele bandia maarufu kama wigi  na kuwataka wahakikishe wanakwenda na nywele zao za asili katika ibada za kanisa hilo

Katika agizo hilo alilolitoa wiki hii, mchungaji huyo aliwataka kuhudhuria ibadani kama walivyo bila kubadili nywele zao  au kutumia dawa au kuvaa nywele bandia

Marekani yenye mchanganyiko wa watu kutoka maeneo mengi duniani  imekuwa na tamaduni tofauti ambapo watu weusi hasa wenye asili ya Afrika wamekuwa wakijaribu kuvaa mavazi tofauti na kubadili nywele zao za asili

Katika mahojiano maalum na tovuti moja ya masuala ya kidini nchini Marekani mchungaji huyo aliyetambuliwa kwa jina la Amir anayeongoza kanisa la Resurrecting Faith huko Waco, Texas aliwaeleza waumini wake kwamba nywele bandia zinawasilisha dhana ya wanawake kutojiamini , kutojitambua na kutojikubali

No comments:

Leave a Reply