Latest News


More

Makubwa! Wahadzabe wanapofunga shule waende harusini

Posted by : Unknown on : Monday, August 12, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
Mkunga huyo anasema mara kwa mara Serikali imekuwa ikipeleka mbegu au zana za kilimo, lakini wao (Wahadzabe) wameishia kuacha vitu hivyo na kuhamia katika mapori yenye utajiri mkubwa wa matunda, mizizi na asali.
Mtuwa anasema serikali inafanya vibaya kuwaamrisha kufanya shughuli za kilimo na kuwapa masharti kuwa wasipolima watakosa misaada muhimu.
“Wanapotuambia tulime na kutupa masharti magumu ni kama wanatuonea. Mizizi na asali ndiyo asili yetu,” anasema.
Afya ya uzazi

Hata katika masuala ya uzazi, Wahadzabe wanaamini kuwa kujifungulia nyumbani ni salama zaidi kuliko katika hospitali. Aya Doffo wa Kijiji cha Sengere anasema katu hataki kujifungua katika hospitali kwani anaamini huko anaweza hata kupoteza maisha.
“Waswahili wanajifungua kwa taabu, wanalala hospitali wakati mwingine wanapasuliwa tumbo, sisi hatutaki hata siku moja kuzalia huko,” anasema Aya kwa Kiswahili cha kubahatisha.
Richard Baallow, ambaye ni kiongozi wa Wahadzabe anasema hivi sasa huduma za uzazi kwa njia ya simu zimewekwa katika maeneo ya Yaedachini na Domanga kwa ajili ya wanawake wanaopata matatizo wakati wa kujifungua.
“Hapa hakuna hospitali, lakini yupo daktari anayetumia ndege (flying doctor) ambaye hufika hapa (Domanga) mara moja kwa mwezi kuwaangalia wanawake wajawazito,” anasema.
Anasema ipo simu maalum ambayo hutumika kumtaarifu daktari huyo aliye katika Hospitali ya Hydom, Wilayani Mbulu pindi linapotokea tatizo wakati wa kujifungua.
Uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia 90 ya wanawake katika vijiji vya Wahadzabe wanajifungua nyumbani, lakini ni wachache wanaopata matatizo ya uzazi.

Ni vigumu kwa Mhadzabe kuumwa na wachache mno wanaopata fursa ya kuonana na tabibu. Hata hivyo, baada ya mwingiliano wa makabila mengine, maradhi kama kifua kikuu yameanza kuwaathiri.

Suala la elimu kwa watu wa jamii ya Wahadzabe bado lina safari ndefu.
Vijana wa Kihadzabe aidha bado hawajaufahamu umuhimu wa elimu au mila na desturi zao zimekuwa ni kikwazo kwako.

(Habari:Mwananchi Communication)


No comments:

Leave a Reply