Latest News


More

Muziki wa Injili bila fedha ni ngumu - Martha Mwaipaja

Posted by : Unknown on : Sunday, September 8, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :


Kuna shairi wa msanii mkongwe hapa nchini lenye maneno; ‘siyo kila ndiyo ina ndiyo kiundani bali kuna ndiyo ambazo siyo zilizojengewa ndiyo bila kufanyiwa uchunguzi’.
 

Shairi hilo liliandaliwa na Fid Q ambaye ni msanii maarufu wa nyimbo za Hip hop nchini kupitia traki yake ya ‘Mwanza Mwanza’. Katika shairi hilo Fid alikuwa akimaanisha kuwa kuna baadhi ya taarifa za uzushi kubadilishwa kuwa kweli na siyo kila uzushi unatakiwa kupuuzwa.

Inawezekana kuna ukweli juu ya waimbaji wa nyimbo za injili kutumika kibiashara, lakini hatua hiyo inaweza kuwa si rahisi kuithibitisha kwa macho bila kuchunguza.

Hatua za kuingia makubaliano na mwimbaji wa nyimbo za injili kwa sasa imedaiwa kuwa ni moja kati ya kero kubwa ambayo siyo wachungaji na waumini wake tu, bali hata jamii isiyoamini dini imekuwa ikihukumu kwa mitazamo hasi.
 

Tuhuma hizo zimezidi kuzagaa kwa kasi kila pembe na duniani kote hali iliyosababisha baadhi ya jamii kuanza kupuuza maana halisi ya kuwepo kwa huduma ya muziki huo. Gharama hizo ni kubwa mno ikidaiwa kuwa kinyume na maagizo ya Mungu.

Hata hivyo sehemu ya Kitabu cha imani hiyo (Biblia) inasema atumikiaye madhabahuni hulia madhabahuni, hoja ambayo pengine imekuwa ikidhaniwa kuchangia mvutano kati ya waimbaji hao na jamii
Matha Mwaipaja ni mwimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini ambaye anakiri wazi kuwepo kwa tuhuma hizo. Anasema hata muziki wa injili unahitaji pesa ili kujiendesha.

“Inafahamika na itabakia wazi kuwa muziki wa injili ni huduma lakini huwezi kufanikisha huduma hiyo bila fedha, gharama za uzalishaji wa nyimbo ni gharama sana, huwezi kurekodi nyimbo bure ni lazima utumie pesa,” anasema Matha.

Wasiojua muziki ndiyo hutuhumu
 

Kwa kile anachokiamini Matha muda wote anasema tuhuma ambazo hutolewa dhidi yao, zinatoka kwa watu wasioufahamu muziki.

“Kwa waimbaji au watu wanaoufahamu muziki huwezi kusikia wakilalamika juu ya dhana kama hizo, watu wanapoona ninapokea kiwango fulani wanadhani ninafaidika sana, sio kweli kabisa,”anasema na kuongeza kuwa;

Siwezi kuwasemea waimbaji wote na siwezi kuthibitisha hizo tuhuma za kutumika kibiashara, lakini niseme tu kwamba katika muziki kuna ugumu wake, wanaotuhumu siwezi kuwanyamazisha kwa dhana ambazo tayari wameshajiaminisha.”.

.............................................Source: Mwananchi Communication..........................................................

No comments:

Leave a Reply