Written by Anonymous

HAPPY NEW YEAR 2015

by Anonymous / 06 Jan 2015

...

Written by Anonymous

MERY CHRISTMAS

by Anonymous / 25 Dec 2014

WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRIS...

Written by Anonymous

HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUZINDUA ALBUM YAO MWEZI APRIL

by Anonymous / 31 Mar 2014

 Kikundi cha Hamugembe Praise and Worship Team cha mjini Bukoba  kinatarajia kuzindua album yao ya nyimbo za kusifu na kuabudu ...

Written by Anonymous

WE WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2014

by Anonymous / 31 Dec 2013

Leo ndio siku ya mwisho kwa mwaka huu 2013 na masaa machache yajayo tutaingia mwaka ujao 2014.Mtandao huu unawatakia kila la kheri na ba...

Written by Anonymous

KWAYA KUU YA USHARIKA WA AZANIA FRONT NDIO MABINGWA WA UIMBAJI WA K.K.K.T – DMP

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Written by Anonymous

MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH LEO

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

KUTOKA MADHABAHUNI

IBADA KATIKA KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE JUMAPILI HII

Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi  (pichani juu) aliongoza na kuhubiri Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa m...

More KUTOKA MADHABAHUNI
More NENO LA LEO
More MAHUBIRI
More MAOMBI

HABARI ZA KIDINI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MHESHIMIWA MAKONDA AZINDUA VITABU VYA INJILI KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE KAWE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe Bwana Makonda (pichani juu) alimsh...

More HABARI ZA KIDINI

More HABARI ZA KIDINI

MWANAFUNZI ANAVYOWEZA KUFANIKIWA VIZURI DARASANI

Posted by : Unknown on : Thursday, September 26, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Fanya Mambo kwa Utaratibu

Unahitaji tu jitihada kidogo ili kupanga mambo kwa utaratibu, lakini unaweza kupata faida nyingi kama vile, kuokoa wakati, kutokuwa na mkazo sana, na kupata alama za juu.

WAZIA umeenda dukani kununua kitu fulani, lakini bidhaa zote zimewekwa ovyoovyo bila mpangilio wowote. Utatumia muda gani kupata kitu unachotaka? Je, haingekuwa rahisi kukipata ikiwa bidhaa zingekuwa zimepangwa kwa utaratibu na vijia vyote vya duka hilo viwe na vibandiko vinavyoonekana waziwazi? Unaweza kutumia utaratibu huohuo kuhusu mambo yako ya shule. Jinsi gani?

Panga ratiba.

“Pindi moja nilisahau kabisa kufanya kazi zangu za shuleni na pia nikasahau kufanya kazi nilizopewa nyumbani kwa sababu nilienda kumtembelea rafiki yangu mwisho juma wote,” anasema Zachary, mwenye umri wa miaka 18, anayeishi Marekani. “Jumatatu, niliwasihi sana walimu wangu wanipe muda wa kumaliza kazi zangu za shule. Sasa mimi huandika orodha ya mambo ya kufanya ili niyakumbuke.”

Kuandika orodha ya mambo ya kufanya pia kumemsaidia Celestine, mwanamke anayeishi Papua New Guinea. Anasema hivi kuhusu wakati alipokuwa shuleni: “Niliandika ratiba ya utendaji wangu wote, kutia ndani kazi za shule, mitihani, na tafrija. Kufanya hivyo kulinisaidia kujua mambo ya kutanguliza na kufanya mambo kwa wakati.”

Dokezo: Andika mambo unayotaka kufanya kwenye kijitabu kidogo, au kwenye simu yako ya mkononi au kifaa kingine cha kielektroniki.

Usiahirishe.

Ni rahisi kusema, “Nitafanya jambo hilo baadaye.” Ni afadhali kufanya mambo mapema iwezekanavyo—hasa kazi za shule.

Dokezo: Uwe na zoea la kufanya kazi za shule mara tu ufikapo nyumbani, kabla ya kuwasha televisheni au kujihusisha katika burudani nyingine yoyote.

Panga vifaa vyako vya shule.

Umewahi kufika shuleni na kugundua kwamba umesahau kitabu au kalamu? Unaweza kuepuka tatizo hilo. Jinsi gani? “Sikuzote mimi huweka vifaa vyangu vya shule kwenye mkoba wangu mapema,” anasema Aung Myo Myat, kijana anayeishi Myanmar.

Dokezo: Weka mkoba wako wa shule ukiwa nadhifu na panga vitu kwa utaratibu ili iwe rahisi kupata kitu unachotaka.

Jambo kuu: Kufanya mambo kwa utaratibu kutakusaidia usisahau vitu, usichelewe, na uwe na wakati wa kutosha wa kufanya mambo mengine yaliyo muhimu.

Anza sasa! Fikiria sehemu ambayo wewe unahitaji kuwa na utaratibu. Kisha mwombe mzazi au rafiki madokezo ya jinsi ya kuboresha sehemu hiyo.

No comments:

Leave a Reply