Latest News


More

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA UZINDUZI WA DVD NA CD

Posted by : Unknown on : Saturday, October 12, 2013 0 comments
Unknown

Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ya Jijini Dar, Emanuely Shedo maarufu kama 'MC Fomafoma' akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tamasha la uzinduzi wa CD na DVD yao ambayo inaenda na kwa jina la 'Namtangaza Kristo' ambayo itafanyika tarehe 13/10/2013 kwenye kanisa lao lililopo Kijitonyama, Dar. Kutoka Kulia kwake ni Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kwaya, Emanuely Shedo alisema nia na madhumuni yao ni kufanya tamsaha la uzinduzi wa kwaya utakaoendana na Jublee.
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na live bendi pamoja na kwaya nyingine ambazo zitaungana nao. DVD na CD zitauzwa siku hiyo pamoja na fulana za 'Namtangaza Kristo' ikiwemo pia Key Holder za Kijitonyama. Msikose watu wote hakuna kiingilio (Itakuwa ni bure kabisa

 

 Wanakwaya wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari.

No comments:

Leave a Reply