Latest News


More

UCHUMI KAMA FURSA KWA MKRISTO KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU - MWINJ.GODILIZEN MOSHI

Posted by : Unknown on : Sunday, October 13, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :


Mwinjilisti Godilizen Moshi (pichani juu) akihubiri  kwenye ibada ya kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge alisema Uchumi ni njia mojawapo mkristo anatakiwa kutumia katika kumtumikia Mungu
Mtumishi huyo alisema katika majuma matatu mfululizo kuanzia jumapili hii atafundisha jinsi mkristo anatakiwa kutumia fursa ya uchumi katika kumtumikia Mungu
Alisema
1.Mhubiri 3: 1 – Kila fursa ya maisha ya mwanadamu imefungwa ndani ya majira na wakati
Kuna umri ukifika huwezi kufanya mambo Fulani hata kama unataka.Alitoa mfano wa elimu huwezi kuanza elimu ya msingi ukiwa na miaka 55 kama kwa kufanya hivyo ni ili ukimaliza shule uweze kuajiriwa kufanya kazi, kwani utamaliza shule umri wa kuajiriwa ukuwa umekwisha
Lazima ujua hata uchumi wako umefungw akwa majira na wakati husika
Aliyebarikiwa katika uchumi ametumia fursa yake vizuri
2.Kusudi la Mungu ni mumfanikisha mwanadamu katika maeneo yake yote
Isaya 48: 17
Mungu amekusudia mwanadamu kufanikiwa kwani neon la Mungu linasema hivyo katika Isaya
Faida uliyopata , unatembea katika misingi ya Mungu alivyokupa?
Ungu anavyokufanikisha unatakiwa na wewe umshirikishe katika mafanikio yako alisisitiza mwinjilisti Moshi




3.Uchumi ni maarifa na ufahamu wa kutumia rasilimali katika kuzalisha
- 1 Falme 17: 10-16
Habari ya mwanamke wa Sarepta na Eliya
Mwanamke ana kiasi kidogo tu cha chakula lakini Eliya nabii anaona fursa aliyo nayo mwanamke huyo
Nabii haoni chakula kidogo bali anaona zaidi ya mwanamke huyu anavyoona
Mwisho tunaona mwanamke huyu anatumia fursa yake sawasawa na anakula na hata kusaza mpaka hali ya njaa inavyoisha kwenye mji aliokua anaishi
JE UNAITUMIAJE FURSA ULIYO NAYO WEWE KAMA MKRISTO? ALIULIZA MWINJILISTI SHAYO

 Picha ya juu na chini waumini wakiwa kwenye ibada ya kwanza kwenye usharika wa Mwenge


Team ya kusifu na kuabudu ikihudumu kwenye ibada ya kwanza

No comments:

Leave a Reply