Latest News


More

JE NI SALA GANI YA BWANA TUNAOTAKIWA KUOMBA?

Posted by : Unknown on : Friday, January 17, 2014 0 comments
Unknown
Saved under : ,

Swali: "Sala ya Bwana ni gani na tunastahili kuiomba?"
Jibu: Sala ya Bwana ni maombi ya Yesu Kristo aliwafunza wanfunzi wake katika Mathayo 6:9-13 na Luka 11:2-4. Mathayo 6:9-13 yasema, “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na Yule mwovu.” Watu wengi wanaelewa vipaya sala ya bwana kuwa sala ambayo tunastahili kukalili neno kwa neno. Watu wengine wanaichukulia sala ya bwana kuwa mbinu ya kiuchawi, kana kwamba maneno yenyewe yako na nguvu au ushawishi wowote kwa Mungu.
Bibilia yafunza kinyume. Mungu ako na haja na mioyo yetu wakati tunaomba kuliko aja aliyo nayo kwa maneno tunayoomba. “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirni atakujazi. Ninyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwakwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Mathayo 6:6-7). Katika sala huwa tunazitoa nyoyo zetu kwa Mungu (Wafilipi 4:6-7), sio kukalilia Mungu maneno tumekalili.
Sala ya Bwana inastahili kueleweka kama mfano, mtindo, wa jinsi ya kuomba. Unatupa “viambato” vinavyostahili kwenda kwa maombi. Hapa ndivyo vile vimegaganywa hadi chini, “Baba yetu uliye mbinguni” yatufunza ni nani tunastahili kumwambia maombi yetu-Baba. “Jina lako litukuzwe” yatuambia tumwabudu Mungu na kumsifu kwa jinsi alivyo. Msemo “Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike humu duniani kama vile mbinguni” ni ukumbusho kwetu kwamba tunastahili kuomba kwa Mungu kuwa mipango yake itimie katika maisha yetu na ulimwengu, sio mipango yetu. Tunastahili kuomba kwa Mungu mapenzi ya Mungu yafanyike, sio haja zetu. Tunasihiwa kuitisha chochote tunachohitaji kutoka kwa Mungu “tupe leo riziki yetu.” “Tusamehe deni zetu, vile tuwasamehevyo wadeni wetu” inatukumbusha kukiri makosa yetu kwa Mungu na kugeuka kutoka kwayo, na pia kusamehe wengine vile Mungu ametusamehe. Tamati wa sala ya Bwana “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu” ni ombi la kusaidiwa ili kupata ushindi juu ya dhambi na ni siaha ya ulinzi kutokana na mitego ya shetani.
Kwa hivyo tena, sala ya Bwana sio maombi tunayostahili kukalili na kumkalilia Mungu. Ni mfano tu peke wa jinsi tunavyostahili kuomba. Je! Kunayo kitu chochote kibaya na kukalili sala ya Bwana? Kawaida hapana. Kunayo makosa yoyote kwa kuomba sala ya Bwana kwa Mungu? La, ikiwa moyo wako uko kwa hayo maombi na kwa kweli wamaanisha maneno uyasemayo. Kumbuka, katika maombi Mungu ako na aja na sisi tunapowasiliana na Yeye tunapoongea kutoka ndani ya moyo wetu, anaangalia meneno tunayotumia. Wafilipi 4:6-7 yasema, “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

No comments:

Leave a Reply