MKRISTO LAZIMA AOMBE WALAU SAA 1 KWA SIKU; ULAZIMA, UMUHIMU WA HILO NA MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA KWA SAA 1 AU ZAIDI… SOMA HII IKUSAIDIE KWENYE MAISHA YAKO YA MAOMBI!
Kiwango Cha Chini Kabisa Cha Muda Ambacho Mungu Anatarajia Mkristo Akitumie Kwenye Maombi “KWA SIKU” Ni “SAA 1″
Mathayo 26:37-44 Inatueleza Habari Ya Yesu Na Wanafunzi Wake Walivyokwenda Bustanini Kuomba; Yesu Aliomba Lakini Wanafunzi Wake Walisinzia.
Alipowajia, Yesu Aliwauliza Swali Lililobeba “KIASI CHA MUDA” Ambao Ni Wa Lazima Kwa Kila Mtu Kuutumia “KWENYE MAOMBI KWA SIKU”
“JE HAMKUWEZA KUKESHA NAMI WALAU KWA SAA MOJA?”
Yesu “ANAKAA KWENYE MAOMBI AKITUOMBEA SISI” (1Yohana 2:1-2, Waebrania 7:25, Warumi 8:34).
Lakini Yesu Anatarajia “KILA SIKU” Mimi Na Wewe “TUTAUNGANA NAYE KUOMBA” Kwa Walau “SAA 1″ Yaani Kama Wanafunzi “WALIVYOKESHA NA YESU” Yesu Anatarajia Kuona Mimi Na Wewe “TUKIKESHA NAYE KILA SIKU KWA WALAU SAA 1 KWENYE MAOMBI”
Inawezekana Huna Uwezo Na Stamini Ya Kuomba “SAA 1 MFULULIZO” Lakini Hiyo Haigeuzi Ukweli Kuwa “YESU ANATAKA KILA SIKU UOMBE NAYE SAA 1 AU ZAIDI” Hata Kama Umebanwa Kiasi Gani, “SAA 1 KATI YA 24 ULIYONAYO, YESU ANATARAJIA ULITUMIE KWENYE MAOMBI PAMOJA NAYE, YAANI UKESHE NAYE KUPITIA MAOMBI”
Ili Kulifanya Hilo Liwezekane, Inahitaji “MBINU ZA MAOMBI” Ambazo “ZITAKUSAIDIA UWEZE KUTUMIA SAA 1 AU ZAIDI KWENYE MAOMBI”
MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA WALAU SAA 1 KILA SIKU NA BWANA YESU:
1.KUOMBA KWA VIPINDI VIPINDI
Unaweza Kuomba Kwa Vipindi Vipindi Kadhaa Kwa Siku. Unaweza Kuomba ASUBUHI NA JIONI, Ama Unaweza Kuomba Mara 3 Kwa Siku Yaani ASUBUHI, MCHANA NA JIONI, Au Unaweza Kuomba Mara 4 Kwa Siku Yaani ASUBUHI, MCHANA, JIONI NA USIKU KABLA YA KULALA!
Jambo La Msingi Ni Kwamba “JUMLA YA VIPINDI VYAKO VYA MAOMBI KWA SIKU VISIWE PUNGUFU YA SAA MOJA; VIWE SAA MOJA AU ZAIDI”
2.KUOMBA KWA KUTUMIA KANUNI YA UFALME WA MUNGU KWANZA
Mathayo 6:33 Inasema “UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE, NA HAYO MENGINE YOTE UYATAKAYO UTAZIDISHIWA”
Hii Mbinu Ni Maalumu Kwa Wale Ambao “HAWANA UWEZO WA KUOMBA SAA MOJA AU ZAIDI” Kwa Kigezo Kwamba “WANAISHIWA MAMBO YA KUOMBEA”
Unapoingia Kwenye Maombi, Anza Kwanza Kuombea “MASWALA YA UFALME WA MUNGU KWANZA KABLA YA KUOMBEA MAMBO YAKO BINAFSI”
-Ombea Huduma Zote Tano Za Kuujenga Mwili Wa Kristo (Waefeso 4:11), Yaani Ombea WAALIMU WA NENO LA MUNGU: Waombee Uwezo Wa Kukaa Barazani Kwa Mungu Na Kuchukua CHAKULA MEZANI PAKE KUKILETA KWA KANISA, Ombea WACHUNGAJI: Waombee Mungu Awape Nguvu Ya KUCHUNGA KONDOO ZAKE, Mungu Awape Nguvu Ya KUTAFUTA MALISHO KWA AJILI YA KONDOO, Mungu Awape Uwezo Wa Kuwajali Na Kuwa Tayari KUTOA UHAI WAO KWA AJILI YA KONDOO, Wasiwe WACHUNGAJI WA MISHAHARA TU BALI WANAOSIMAMIA MASLAHI YA UFALME WA MUNGU Nakadhalika, Ombea WAINJILISTI: Mungu Awape Roho Ya Hekima, Ufunuo Na Uweza, Ili WAIHUBIRI SIRI YA WOKOVU KWA UJASIRI NA NGUVU, HUKU ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA IKIFUATANA NAO… Ombea MANABII WA KWELI WA MUNGU: Mungu Awatetee Na Kuwapigania Mbele Ya Kila Mbinu
Na Mpango Wa Adui Kujaribu Kuwapinga Na Kuwazuia, Mungu Azidi Kufungua Macho Na Masikio Ya Mioyo Yao Ili Wapokee PACKAGE ZA WATU, NCHI, KANISA Nakadhalika… Ombea MITUME, Mungu Awatumie Kufika Maeneo Ambako Kazi Ya Mungu Haijafika Na Wakaanzishe Kule Kazi Na Zisimame Na Kutoa Matunda!
UNAPOOMBA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU; USIOMBEE KANISA/ DHEHEBU LAKO TU, OMBEA MAKANISA NA MADHEHEBU YOTE YANAYOSIMAMIA KAZI ZA UFALME WA MUNGU!
-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
Ombea Watu Ambao WAMESHAOKOKA WASIMAME: Kwa Kuwaombea Wengine, UNAMFANYA MUNGU AKULINDE WEWE USIMAME KWENYE WOKOVU, Maana Kipimo Unachopima UNAPIMIWA!
-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
Ombea UMOJA WA KANISA: Mitume Wawe Na Umoja Kihuduma, Manabii Wawe Na Lugha Moja, Walimu Wasimame Pamoja Na Kwa Umoja, Wainjilisti Wafanye Kazi Ya Injili Pasipo Mashindano Bali Kwa Upendo Na Umoja, Wachungaji Wapendane, Wawe Wamoja Na Wasiwe Na Mashindano… Kwa Kuwaombea WATUMISHI, UNAFUNGULIA MLANGO WA UMOJA, NA KUIZUIA ROHO YA UDINI NA UDHEHEBU NA KUINUA BENDERA YA YESU!
-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
OMBEA AMBAO HAWAJAPATA NEEMA YA WOKOVU ILI NAO WAOKOLEWE: Kwa Kuombea Walioko Dhambini, Unamfungulia Mlango Mungu Kukusaidia Ili Wewe Usirudi Dhambini… Kwa Kuombea Ambao Hawajapata Neema Ya Wokovu Utakuwa Umefungulia Mlango Kwa Mungu Kuwaokoa Ndugu Zako, Marafiki, Jamaa Zako Ambao Hawajaokoka… Usisahau Yesu Alisema, “ANYWESHAYE NAYE ATANYWESHWA”
-Kwenye Kuombea Kipengele Cha Ufalme Wa Mungu;
KABLA YA KUOMBEA MAHITAJI YAKO KWANZA WAOMBEE WANA WA MUNGU WENGINE WALIOKO KWENYE SHIDA AU UHITAJI KAMA WAKO: Kwa Kufanya Hivyo Utakuwa UMEOMBEA VIUNGO WENGINE WA MWILI WA KRISTO, Na Mungu Atainua Watu Wa Kukuombea Na Wewe Pia, Lakini Pia UTAMFANYA MUNGU AONE UPENDO WAKO HALAFU ATAKUGUSA WEWE KWANZA HATA KABLA HUJALISEMA LAKO MBELE ZAKE!
(Source: Yesu ni bwana.org)
No comments: