KWANINI NI MUHIMU KWENDA KANISANI?
Posted by :
Unknown
on :
Friday, January 24, 2014
0 comments
Jibu: Bibilia yatuambia kwamba twastahili kuenda kanisani ili tukaweze kumwabudu Mungu pamoja na washirika wengine na tufunzwe neno lake ili tuwe kiroho (Matendo Ya Mitume 2:42; Waebrania 10:25). Kanisa ni mahali ambapo waumini wanaweza kupendana (1 Yohana 4:12), tianeni moyo ninyi kwa ninyi (Waebrania 3:13), “tianeni” moyo ninyi kwa ninyi (Waebrania 10:24), tumikianeni (Wagalatia 5:13), onyaneni ninyi kwa ninyi (Warumi 15:14), heshimianeni ninyi kwa ninyi (Warumi 12:10), iweni wafadhili, na huruma ninyi kwa ninyi (Waefeso 4:32).
Wakati mtu anapomwamini Yesu Kristo kwa wokovu, huyo mtu amefanywa mshirika wa mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:27). Ili mwili wa kanisa ufanye kazi vizuri, “sehemu” zake zote zinastahili kuwepo (1 Wakorintho 12:14-20). Vilevile Mkristo hafiki upeo wa kukua kiroho bila ya usaidizi na utiaji moyo wa wakristo wengine (1 Wakorintho 12:21-26). Kwa sababu hizi,kuenda kanisani na kushiriki katika kazi za kanisa, na ushirika ni vitu vya kila wakati kwa maisha ya mkristo. Kuenda kanisani kila juma si muhimu au “lazimisho” kwa muumini, lakini kwa mwenye akonani ya Yesu lazima awe na nia ya kumwabudu Mungu, alipokee neno lake na kuwa na ushirika na wakristo wengine.
Saved under :
Habari za Kidini,
Mahubiri
No comments: