Written by Anonymous

HAPPY NEW YEAR 2015

by Anonymous / 06 Jan 2015

...

Written by Anonymous

MERY CHRISTMAS

by Anonymous / 25 Dec 2014

WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRIS...

Written by Anonymous

HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUZINDUA ALBUM YAO MWEZI APRIL

by Anonymous / 31 Mar 2014

 Kikundi cha Hamugembe Praise and Worship Team cha mjini Bukoba  kinatarajia kuzindua album yao ya nyimbo za kusifu na kuabudu ...

Written by Anonymous

WE WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2014

by Anonymous / 31 Dec 2013

Leo ndio siku ya mwisho kwa mwaka huu 2013 na masaa machache yajayo tutaingia mwaka ujao 2014.Mtandao huu unawatakia kila la kheri na ba...

Written by Anonymous

KWAYA KUU YA USHARIKA WA AZANIA FRONT NDIO MABINGWA WA UIMBAJI WA K.K.K.T – DMP

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Written by Anonymous

MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH LEO

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

KUTOKA MADHABAHUNI

IBADA KATIKA KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE JUMAPILI HII

Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi  (pichani juu) aliongoza na kuhubiri Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa m...

More KUTOKA MADHABAHUNI
More NENO LA LEO
More MAHUBIRI
More MAOMBI

HABARI ZA KIDINI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MHESHIMIWA MAKONDA AZINDUA VITABU VYA INJILI KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE KAWE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe Bwana Makonda (pichani juu) alimsh...

More HABARI ZA KIDINI

More HABARI ZA KIDINI

Mwafrika kuenda anga za juu

Posted by : Unknown on : Tuesday, January 28, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :


DJ Mandla Maseko




DJ mmoja mwenye umri wa miaka 25 nchini Afrika Kusini anatarajiwa kuwa mwafrika wa kwanza kufika katika anga ya juu zaidi.



Mandla Maseko ni mmoja wa watu 23 ambao wamejishindia nafasi ya kuweza kufika katika anga ya juu mnamo mwaka 2015.



Anafafanua alivyowashinda watu milioni moja kutuzwa nafasi hiyo.



''Anga sasa inafikika-ilikuwa ni kama ndoto ya mbali kwa watu kama mimi.Sasa hivi inawezekana na natumai watu watazidi kujihusisha nayo.



Nilitaka kufanya jambo lisilo la kawaida-Napenda kujaribu mambo mapya na hii ilikuwa fursa nzuri kwangu.



Mwanzoni niliona tangazo la kibiashara la shindano hilo kwenye runinga na baadaye kwenye redio.Nilihitajika kutuma picha yangu nikiruka kutoka popote pale.Hivyo basi nikaruka kutoka ukuta mrefu na rafiki yangu akanipiga picha nusu hewani.



Nilitakikana pia kujibu maswali na kueleza kwa nini nilitaka kutalii anga ya juu.Jibu langu lilikuwa;’Nataka kuvunja sheria za uzito na kuandikwa kwenye vitabu vya historia kama mwafrika wa kwanza kutua angani’



Nilikuwa mmoja wa watu thelathini waliochaguliwa kuenda katika kambi ya anga iliyoko Parys,Free State.Nilihitajika kupitia majaribio matatu-mawili yakiwa ya lazima.Moja ilikuwa kuruka kutoka futi 10,000 hadi kwenye ardhi na nyingine ilikuwa ni tapiko la nyota wa mkia.

Mimi kama kijana wa vitongojini nilijifunza kukabiliana na majaribio yoyote ninayopewa bila ya kusita



Tapiko la nyota ya mkia ilikuwa ni chumba ambapo ulihitajika kusimama kando ya ukuta ,kisha ilianza kuzunguka kisha ulipofika hatua fulani sakafu inapotea,hivyo basi unabakia kusukumwa kwenye ukuta na mvuto wa dunia.Changamoto ilikuwa kuokota bendera tano kutoka chini ya miguu yako na kuviweka kichwani.



Nilifuzu jaribio hilo, hivyo basi kundi lilipunguka hadi watu sita na tulihitajika kufanya tuliloita”Plane Stunt”



Tulisafirishwa hadi futi 3,000 ama 4,000 kupitia ndege kisha rubani alifanya michezo za hewani kwa ustadi kama vile kupiga duara na kupinduka.



Tuliposhuka kwenye ndege,tukiwa tunaogopa lakini tulijitahidi kuwa watulivu kwa kuwa papo hapo tulihitajika kufanya mtihani kuelezea jinsi safari hiyo ilivyokuwa.




Lynx



Niliweza kuwa kati ya watatu bora hivyo basi tulisafiri kwa ndege hadi Orlando,Florida tarehe mosi Disemba. Huko tulikutana na washindani wengine 109 kutoka pande zote za dunia.



Tulishiriki katika majaribio mengine yaliyokuwa magumu sana,lakini mimi kijjana wa mjini ;nilifunzwa kukabili jaribio lolote bila kusita, na hivyo ndivyo nilivyofanya.Tulihitajika kufanya majaribio mengine na nikazikamilisha vizuri.



Walipotangaza washindi,na jina langu likatajwa ,sikuwa tayari,hivyo basi nilipofahamu kwamba jina langu lilikuwa limeitwa, mwili wangu ulijawa na joto.Hadi leo,sijaweza kufahamu vizuri.Nafikiri nitaifahamu vyema dakika nitakapopaa angani.



Nitakwenda na bendera yangu ya Afrika kusini ilio na ramani ya Afrika.Pia nataka kwenda na wimbo ulioimbwa na PJ Powers na Ladysmith Black Mambazo unaoitwa World in Union.’Ikiwa nitashinda au kushindwa,itakuwa ni ushindi kwa wote.umoja duniani,dunia kama moja.Tunapoelekea kutimiza malengo yetu,kizazi kipya kimeanza.’haya ndiyo maneno ya wimbo huu.

Nitacheza wimbo wa taifa pia nitakapokuwa napaa.


Washindi watakaosafiri kwenda angfa za juu na Maseko



Familia na marafiki wangu wote wamenipongeza. Nilizaliwa na kulelewa katika miji ya Mabopane na Soshanguve ,hivyo basi mimi ni Mwana Pretoria kamili.Namshukuru babangu kwa kuhakikisha sikulala njaa au nje hata siku moja.



Na kwa mamangu ambaye mara nyingi ningehudhuria mashindano na kufeli angenishauri kuwa,”Ah,usijali,kitu kikubwa kinakujia,huu haukuwa wakati wako.”



Ningemjibu kwamba,”Ah we ni mamangu,haupaswi kusema mambo kama hayo.”Lakini jambo likitokea,kama vile mimi kupaa angani nasema ,Mama kweli alisema.”Huu ni ushindi mkubwa.”



Kwa kawaida,tunaskia mambo kama hayo yakitimizwa na watu wasio wa karibu, lakini inapokuwa mtu unayeweza kujihusisha naye,ni jambo la kufurahia mno hivyo basi watu waliokaribu nami wamefurahi sana.



Nasimamishwa njiani na watu wanaonipongeza.



Nilitaka kufanya jambo ambalo lingewatia moyo vijana wa Afrika Kusini na Afrika kwa jumla,na hata vijana duniani kote kwa kadri nitakavyoweza.Nataka kuonyesha kuwa haijalishi ulikotoka,unaweza kupata chochote utakacho ikiwa utatia bidii.



Baada ya kupaa angani natarajia nije nikamilishe masomo yangu ya uhandisi.



Ninatarajia pia kusomea elimu ya wanahewa na natumaini kufuzu kama mjumbe mtaalamu,ili wakati ujao nitue kwenye mwezi na kupandisha bendera ya Afrika Kusini kule.''

No comments:

Leave a Reply