Latest News


More

PAPA FRANCIS AWATAKA VIONGOZI KUJALI

Posted by : Unknown on : Wednesday, January 22, 2014 0 comments
Unknown
Kiongozi wa kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito kwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kimataifa mjini Davos kuhakiksiha kuwa mali na utajiri ulio hapa duniani unapaswa kuwahudumia raia badala ya kuwatawala.
Papa huyo kutoka Brazil, amekuwa mkosoaji mkubwa wa mfumo ubepari ambao unawakandamiza watu walio masikini na amekuwa katika mstari wa mbele kutetea maslahi ya raia wa nchi hiyo ambao wengi wao ni masikini.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba ya papa na Kadinali Peter Turkson, kutoka Ghana, ambaye ni mkuu wa tume ya haki na amani huko Vatican, Papa Francis, amewaomba wafanyabiashara katika mkutano wa kimataifa wa kiuchumi kuusaidia umma, badala ya kuruhusu umaskini usambae duniani.

Kuondoa umasikini duniani
Papa Francis alitoa wito kwa viongozi hao kujitolea zaidi na kufanya mengi zaidi kuliko kuzingatia maslahi ya kawaida na pia kutathmini jinsi kuhakikisha kuwa utajiri wa taifa umesambazwa kwa raia wote.
Wakati huo huo amewarai wafanyabiashara kuchukua jukumu hilo huku wakiwa na mtizamo na mwelekeo wa kuimarisha hali ya maisha duniani.
Mapema wiki hii shirika la Oxfam, liliripoti kuwa watu themanini na watano tajiri zaidi duniani, wanamiliki utajiri ambao ni sawa na mali inayomilikiwa na zaidi ya watu bilioni tatu na nusu wengi wao wakijumuisha nusu ya watu walio na mapato ya chini zaidi duniani.
Amesema ukuaji wa usawa ni zaidi ya ukuaji wa kiuchumi licha ya kuwa vyote vinaambatana.

No comments:

Leave a Reply