Huduma ya New Life in Christ ya jijini Dar es salaam ikishirikiana na Mwalimu Christofa Mwakasege jumapili iliyopita iliandaa semina ya neno la Mungu ya kupanda na kuvuna ambayo ilifanyika siku ya jumapili ya tarehe 12/01/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga jijini Dar es salaam
Semina hiyo iliyofanyika kuanzia saa 7 kamili mchana na kuendelea ilihudhuriwa na mamia ya waumini wa dini mbalimbali toka katika jiji la Dar es salaam na nje ya jiji hili ambapo mnenaji mkuu katika semina hiyo alikua mwalimu Christofa Mwakasege.Pia kulikuwepo na waimbaji mbalimbali wa sifa kama vile Praise and Worship Team, Kwaya na waimbaji binafsi walikuwepo wakimsifu Mungu katika roho na kweli.
Waumini wengi waliohojiwa na mtandao huu wa tumainiletu walifurahia semina hiyo na wengi walitamani iwe inafanyika angalao mara moja kwa mwezi
Mtandao huu wa tumainiletu.com unawatakia kila la kheri huduma ya New Life in Christ ili waweze kuandaa semina nyingine kama hii
"SIFA NA UTUKUFU NI KWA BWANA!!
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: