Shirika la umoja wa mataifa la Utamaduni , UNESCO, limeonya kuwa viwango vya chini vya elimu duniani vinawakosesha watoto uwezo wa kusoma
Shirika la umoja wa Mataifa la UNESCO, limesema kuwa viwango vya chini vya elimu katika nchi nyingi duniani vinawakosesha watoto uwezo wa kusoma.
Katika ripoti yake iliyoiita ''elimu kwa wote'' , UNESCO inasema dola bilioni 129 zilipotea katika utoaji wa elimu duni.Ripoti hiyo inasema kuwa iwapo waalimu wa kutosha hawatavutiwa na taaluma hiyo na kupewa mafunzo , basi viwango vya chini vya elimu vitaendelea kwa vizazi kadhaa.
Ripoti hii inatolewa wakati nchi nyingi zinazostawi zikionyesha juhudi za kuboresha elimu .
Mfano ni nchini Kenya ambako Kuanzishwa kwa elimu bila malipo katika shule za msingi kunaonekana kama mchango wa kufikia lengo la pili la milenia, ambalo ni kuhakikisha kufikia mwaka ujao, watoto kote watakuwa wana uwezo wa kumaliza masomo katika shule za msingi.
.Lakini kama anayotuarifu Maryam Dodo Abdalla, uwekezaji huu bado haujadhihirisha jukumu muhimu la elimu ya msingi katika maendeleo.
No comments: