Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mwinjilisti Jonas Gwemelu (pichani juu) wa Usharika wa Wazo alisema katika somo la wiki iliyopita tulijifunza mambo yafuatayo katika utoaji
1.Kwa nini tunatoa sadaka
2.Kwa nini Mungu anaruruhusu tutoe sadaka
3.Sifa ya mtoaji wa sadaka
Utoaji wa sadakani ile hali ya kutambua kwamba kila ulicho nacho chatoka kwa Mungu
Hivyo unapotoa unamrudishia Mungu utukufu na kuonyesha shukrani kwake
Kut 25:1-9
Mungu anapokutana na wewe hakutani na wewe tu bure kwani kuna kitu anataka kukifanya juu au ndani yako
Mat :5 – Inatufundisha kuwa watu walitoa sadaka isiyomfurahisha Mungu.. hii inaonyesha kuwa si kila sadaka Mungu anaipokea
Sadaka ni kitu muhimu kwa Mungu
Luka 12:32
Hapa Yesu anaangalia sadaka kama kitu cha thamani kuliko vitu vyovyote alivyo navyo mwanadamu
Anawashauri watu wauze walivyo navyo vyote watoe sadaka; ina maana vyote walivyo navyo wanadamu havina thamani yoyote kama sadaka
Hagai 1: 6-7
Sadaka inategemea nguvu kwa mtoaji na kumpa Baraka
Yesu anasema viuuzeni vyote mlivyo navyo mtoe sadaka na msijifanyie mifuko isiyochoka
Unapotoa sadaka ni kama unaweka akiba ya baadaye itakayokusaidia kuja kutimiza malengo yako ya baadaye
Mfano wa Kornelio;Mungu aliona Kornelio ana shida akamwambia sala zako na sadaka zako zimenifikia alisema mwinjilisti Jonas
Mwinjilisti Jonas alisema unapotoa sadaka unaweka maisha yako ya kiroho mahali pa salama
Ibada hiyo iliongozwa na mwinjilisti wa usharika wa Mwenge mwinjilisti Mwigune na somo lilifundishwa na mwinjilisti Jonas Gwemelu toka usharika wa Wazo
Washarika wakiwa kwenye ibada hiyo ya jumapili katika Usharika wa Mwenge
Washarika wakiwa kwenye ibada hiyo ya jumapili
No comments: