Latest News


More

YESU KRISTO NI BWANA WA HURUMA

Posted by : Unknown on : Monday, March 31, 2014 0 comments
Unknown



Zaburi: 119:41-48

Neno la Waraka: Wafilipi. 2:10-11

Neno Kuu: Mathayo 14:13-21

Yesu Kristo alifanya kazi ntingi hapa duniani na nyingi ni miujiza ambayo hakuna binadamu anayeweza kuifanya.Akihubiri katika ibada ya jumapili ya jana mchungaji Simon Fue (pichani juu) alisema nguvu na kazi za miujiza alizozifanya Yesu Kristo ilionyesha uwezo wa kimungu ambao alikua nao haswa pale ambapo mwanadamu amefikia ukomo wa kufikiri hapo ndipo uwezo wa Mungu unapoonekana

Wanafunzi wa Yesu walikata tama haswa walipoangalia mikate michache na samaki wachache waliokua nao na kundi kubwa la watu waliokua pale kwenye makutano, na Petro alimwambia Yesu kwa mikate na samaki hawa wachache vitafaa au kutosha nini?

Yesu Kristo anapokea mikate 5 na samaki 2 anaibariki na kumshukuru Mungu na katuika kutumia anasema vitumike jinsi ya Kimungu na kwa utukufu wa Kimungu

Katika kugawanya au kuwagawia watu; wanafunzi wanashangaa havikuisha na kila mmoja anakula na kushiba mpaka wakasaza tena vinajaa vikapu 12

Katika muujiza huu tunajifunza kuwa Yesu Kristo ni bwana wa huruma

Katika hali ya kukata tama, kukosa amani, kukosa chakula, kudharauliwa n.k bwana anakutia moyo na kukuhurumia na hajakuacha , yui pamoja nawe.

Waweza kuona kwamba anachelewa kukujibu lakini Mungu ana wakati wake wa kujibu maombi yetu; hivyo usichoke au usikate tama



Muujiza wa bwana huanza pale unapomshukuru Mungu kwa kile alichokupa.Shukrwani ni muhimu sana kwa Mungu na hapo ndipo muujiza wako unapoanza alisema mchungaji Fue

Tafakari kwanza yale ambayo Mungu amekupa na yanayokuzunguka na kasha mshukuru Mungu

Mara nyingi wanadamu wanakosa muujiza wa Mungu kwa kutokushukuru hata kwa kile kidogo walicho nacho

Wanafunzi wa Yesu walikata tama haswa kwa vile waliona kundi kubwa na mikate na samaki wachache waliokua nao

Yakupasa kushiriki vyote ulivyokwisha pokea; japo ni kidogo au vingi mshukuru Mungu

Pale mtu anapoamua kushiriki kidogo ulicho nacho na wengine hapo ndipo muujiza wa bwana unapotokea

Mshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo Mungu amekufanyia kiwe kidogo au kikubwa

Hakuna kinachoweza kukutosha kama neema ya Mungu haiku ndani yako

Yesu Kristo anasema aulaye mwili na damu yake anao uzima wa milele

Baraka zote za mwili , za kiroho , kwamba ni kidogo au kingi ni mfano halisi wa maisha ambayo Mungu ametupa

Imetupasa kuweka Tumaini letu kwa Yesu Kristo ndipo kuula na kushiriki na bwana Yesu Kristo alimaliza mchungaji Fue

Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi na mwinjilistio wa Usharika mwinjilisti Mwigune

No comments:

Leave a Reply