WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imeshathibitisha kuhusiana na ujio wake kwenye tamasha hilo.
Ephraim Sekeleti
“Tunafurahi kwamba tamasha letu mwaka huu Dar es Salaam mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mwaka jana alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe,” ilisema taarifa hiyo ya Msama.
Sipho Makabane
Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo, ambapo wan je ya nchi ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda.
Solomon Mukubwa
Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro, Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.
John Lissu
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
No comments: